Nawezaje kupata pesa za mkopo ili niendeleze uwekezaji wangu?

likat

Member
Joined
Feb 19, 2013
Posts
40
Reaction score
32
Nahitaji ushauri. Mimi ni entreprenuer ninayeanza. Nategemea kujishughulisha na utengenezaji wa vyakula vya mifugo na pia uchakataji wa mafuta ya kupikia katika hatua ya " refining". Nimesha install machine kwa ajili ya uwekezaji. Kiufupi nimewekeza Tsh 100,000,000 kama physical capital hasa upande wa machines ila ninahutaji wa operating capital kwa ajili ya kuanza uzalishaji.

Changamoto kubwa kila mahali ninapoenda kuomba fedha hasa mkopo wananiambia biashara yangu inatakiwa iwe ina mwaka 1 na inazalisha mapato ukiangalia mimi ndio ninaanza. Machines ninazo nimeshafunga kwa ajili ya kuanza kazi, umeme nimeingiza, majengo ninayo lakini kupata fedha ni shida sana. Machine zipo 6.

Wadau ninaomba ushauri wenu, mawazo yenu.

20240703_111100.jpg
 
Dah! Pole sana. Nchi yetu ingekuwa ina sera nzuri ya kuwadhamini wawekezaji wazawa, nadhani mpaka sasa ungekuwa tayari umeshapata suluhisho. Ila ndiyo hivyo tena.

I wish ungekuwa hujanunua hizo mashine zote 6, ningekushauri uanze kwanza na mtaji mdogo, halafu baada ya biashara kuchanganya ndiyo ungeenda sasa benki kwa lengo la kuongeza mtaji.
 
Asante sana mkuu, ni kweli kabisa sera za kuinua early stage sme,s Tanzania hakuna.
 
Umeanza biashara bila kua na plan nzuri. Ungefanya vitu vifuatavyo ungeupiga mwingi sana

1. Ungeanza na machine za kawaida kwanza, ambazo biashara yako itakua inakua taratibu

2. Sajili biashara yako kwenye mamlaka husika, ikiwemo Brela, TRA, Tafuta Leseni ya biashara, fungua akaunti ya benki unayotaka kukopa, Anza kupiga kazi. Kila pesa inayopatikana kwenye biashara yako hakikisha inapita kwenye hiyo akaunti.

3. Hakikisha una dhamana inayoenda thamani na pesa unayotaka kukopa.

N.B. Hakikisha biashara yako unairasimisha na unalipa kodi kwa wakati
 
Asante kwa ushauri.
 
Back
Top Bottom