Nawezaje kuwa freelancer hapa Tanzania?

Nawezaje kuwa freelancer hapa Tanzania?

Unahitaji skills ili uwe freelancer.. lakini ili uwe Freelancer mzuri unahitaji uwe na sifa hizi.

1. Ujue kuifanya kazi yako vizuri kuliko watu wengine wengi ( usikubali upitwe ujuzi na watu wengi )

2. Tengeneza portfolio ( anza kufanya kazi bila malipo au kwa malipo ya chini na uzifanye kwa juhudi zote )
Hii itakusaidia kupata wateja wa awali na kupata kazi za kuwaonesha wateja wa baadae )

3. Tengeneza portfolio na utumie mitandao ya kijamii kujitangaza na kuonesha kazi zako.

4. Tengeneza connection na waajiriwa, freelancers wenzako, middlemen, managers na mtu yeyote ambae ataitambua kazi yako na ataweza kukupa kazi hapo baadae

5. Communication skills ni lazima, uwe unaweza kuwasilisha mawazo yako kwa lugha ya kiswahili na kiingereza.

6. Jali muda, fanya kazi kwa muda, muda ndio pesa yako wewe kama freelancer sababu utakuwa unafanya kazi na bosi zaidi ya mmoja na wote watataka kazi wazipate kwa muda sahihi.

7. Kuwa na msimamo, usifanye kazi kwa tamaa ya pesa ndogo ndogo.. utaishia kuharibu kazi za watu. Jiwekee bei yako na uwe na msimamo na bei yako

8. Usiache kujifunza kila siku, kuwa mbunifu, jaribu vitu vipya.. usiwe comfortable kabisa.

Vitu ni vingi ila nilivyolist hapo vinatosha kuanza navyo.

Kuna skills nyingi kama Photography, Videography, Video Editing, VFX & 3D.
Motion Graphics, Graphics Design, Web Design, Web development, Mobile App Development, Writing, Marketing, Social Media Management, Digital marketing, etc.
 
Back
Top Bottom