Nawezaje kuwadhibiti mchwa wanaoharibu nyasi?

Nawezaje kuwadhibiti mchwa wanaoharibu nyasi?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Jitihada kadhaa zimeshafanyika bila mafanikio.

Zilipoanza kutafuna nyasi za "garden", ilisemekana kukimwagiliziwa kila siku hilo tatizo litaisha. Hilo limekuwa likifanyika tokea mwaka Jana lakini halijasaidia.

Nilipoenda duka la pembejeo, nilipewa dawa inayoonekana hapo chini. Imeshapuliziwa zaidi ya mara moja lakini mchwa bado wameendelea kuzifaidi nyasi ambazo hawajzitolea jasho.

Naomba wajuzi mliomo humu mnipe mbinu ya kuweza kuwatokomeza hao viumbe bila kung'oa nyasi.

Asanteni.

IMG_20240209_113824_773.jpg
IMG_20240209_113818_201.jpg
IMG-20240209-WA0002.jpg
 
Okay. Basi jaribu kuonana na wataalamu wa garden ata kama ni jamaa local. Wanakuaga wanauza na maua kwenye zile pots watakusaidia.

Mi niliwatumia watu wa gardeni walitoa msaada mkubwa ingawa changamoto zetu zipo tofauti.
Shukran sana mkuu🙏
 
Kuna mimea fulani ukipanda mizizi yake ni repellant ya mchwa ila siku hizi watu wamekuwa waharibifu wa mazingira inapotea sana, ilikuwa inapatikana ukanda wa ubenani kuelekea usangu
 
Inaitwaje mkuu na picha kama unayo
Ukipata mtu aliyepo mitaa ya Ilembula Njombe akawauliza wenyeji wanaijua bad luck niliondoka huko kitambo

Nimejaribu kutafuta picha yake naukosa ila mizizi yake ni michungu balaa wengine huitumia kama dawa ya typhoid
 
Jitihada kadhaa zimeshafanyika bila mafanikio.

Zilipoanza kutafuna nyasi za "garden", ilisemekana kukimwagiliziwa kila siku hilo tatizo litaisha. Hilo limekuwa likifanyika tokea mwaka Jana lakini halijasaidia.

Nilipoenda duka la pembejeo, nilipewa dawa inayoonekana hapo chini. Imeshapuliziwa zaidi ya mara moja lakini mchwa bado wameendelea kuzifaidi nyasi ambazo hawajzitolea jasho.

Naomba wajuzi mliomo humu mnipe mbinu ya kuweza kuwatokomeza hao viumbe bila kung'oa nyasi.

Asanteni.

View attachment 2901755View attachment 2901756View attachment 2901757
Jaribu kutrace kama kuna kichuguu karibu au sehemu wanapotokea anzia mashambulizi hapo maana ndio malkia yupo kula au kushambulia garden yako ni kwenye utafutaji tu wa chakula utamwaga dawa ikupungua nguvu watarudi tena kushambulia.
 
Ukipata mtu aliyepo mitaa ya Ilembula Njombe akawauliza wenyeji wanaijua bad luck niliondoka huko kitambo

Nimejaribu kutafuta picha yake naukosa ila mizizi yake ni michungu balaa wengine huitumia kama dawa ya typhoid
Ngoja niulize
 
Tafuta dawa iitwayo DRUGNET (ndio dawa rasmi ya mchwa ninayoijua) unanikumbuka.
 
Eleza uliweka dawa kiasi gani kwenye maji kiasi gani Ili usaidiwe na ulipiga mara ngapi ? Na eneo Lina ukubwa Gani ukinijibu hayo na kama uko tayari nipe kazi hiyo maana ndo kazi zetu hizo kuanzia kumeneji viwanja vikubwa(Turf management), mbegu za ukoka na mengineyo. Tatizo lako limeshapata suluhisho hilo
 
Kuna mimea fulani ukipanda mizizi yake ni repellant ya mchwa ila siku hizi watu wamekuwa waharibifu wa mazingira inapotea sana, ilikuwa inapatikana ukanda wa ubenani kuelekea usangu
Mkuu hizi chemical kama synthetic fertilizer yameua udogo na viambatanisho vyake kama microbes,zamani tulikuwa hatuhitaji dawa za kunyunyizia wadudu,sasa hakuna kinga ni chemical kutokea round up,mbegu yenyewe ina machemical,mbolea za kupandia nazo machemical,maji yana machemical,viatilifu ni chemical,nawe ukila zao lake ni chemicals ndio sababu maradhi hayatuachi salama.
 
Back
Top Bottom