Adolph Jr
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 5,950
- 9,511
Wasalaam wanajukwaa,
Ilikuwa mwaka jana (2021) mwezi wa tisa nilipochukua fomu ya Tanesco kuomba kufungiwa umeme kwangu, walinipatia bila masharti yeyote nilijaza na kuwarudishia tatizo lilianzia kutumiwa "control number". Walinizungusha sana hadi mwezi February mwaka huu(2022) ndiyo walinitumia sikuona ajabu maana hili shirika kulaumiwa kwao ni kawaida.
Sasa kisanga kikuu ni baada ya kulipia huo mwezi wa pili hadi leo hii tarehe 10/06/2022 mambo bila bila.
Nikiwapigia simu wanasema niendelee kusubir, hivi hii imekaaje kusubiria umeme karibia mwaka mzima ni haki kweli? Na je Watanzania wote nao wanapitia adha kama hii na wako kimya tu?
Mimi nimeamua kutafuta njia nyingine.
1: Naomba kufahamu namna ya kuwasiliana na Rais,Waziri mkuu au waziri anayehusika na nishati niwasilishe dukuduku langu..hasa hasa kwa email.
2: Ikishindikana naomba kufahamu namna ya kulifungulia mashtaka (mahakamani) shirika hili kwa kunipotezea muda wangu wa kwenda wilayani kufuatilia umeme na pia kunikoshesha kipato maana nilikuwa nina mpango wa kufungua biashara hapa kwangu inayohitaji umeme.
3: Mwisho nitashukuru kwa msaada wenu wa kufanikisha suala hilo.