Nawezaje / Tunawezaje kuuza nje mazao ya yatokanayo na kilimo

Nawezaje / Tunawezaje kuuza nje mazao ya yatokanayo na kilimo

The Knowledge Seeker

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2019
Posts
3,418
Reaction score
5,028
Habari wana jamii wenzangu. Kama kichwa cha habari kilivyojieleza hapo juu. Nimekaa nakutafakari namna na jinsi ambavyo ninaweza, au tunaweza kama vijana kutafuta masoko ya mazao yatokanayo na kilimo nje ya nchi. Mfano wa uchache wao ni kahawa, korosho, pamba karafuu na mengineyo

Kwenye utafiti wangu mdogo, nmeamua kujikita kwenye kahawa. Kahawa ni zao linalolimwa kwa wingi Tanzania, na ukienda kwenye vyama vya ushirika unakuta kuna stoku kubwa, au shehena na shehena, za aina au gredi mbalimbali za kahawa. Sasa utajiuliza ni kweli wateja wa hizi kahawa hawapo au msimu huu kahawa imevunwa kwa vingi kuliko mahitaji ya soko...

Ukienda south Africa huko unywaji wa kahawa ni mkubwa kutokana na lifestyle ya huko, sasa kama ukiwa unatembea katika supermarket utakuta kahawa ambayo iko inauzwa hapo ni nyingi kutokata Brazi, Vietnamese, Italy, mpaka huko Guatemala. Lakini si kwamba hawanunui toka Tanzania. Wananunua kama vile wanunuavyo katika masoko mengine na wanai processed na kuiuza tena kwenye masoko yao ya ndani na nje ya nchi pia. Ukitembelea katika website ya Alibaba, huko utakuta kahawa mbalimbali katika grade's mbalimbali kutoka katika nchi zilimwazo kahawa, lakini hutakutana na hata sellers yeyote aliyejiorodhesha kama muuzaji kutokea Tanzania.

Nikiwa kama kijana au vijana, nijukumu langu kujua ni namna gani au jinsi gani naweza kuyapatia wateja mazao yote yanayokanayo na kilimo, ndani na pia nje ya nchi kwa lengo lakuisaidia serikali, nchi na wananchi kwanamna moja au nyingine. Katika kila fursa kuna changamoto, na katika kila changamoto kuna fursa vilevile.

Ijapokuwa katika uuzaji wa mazao nje ya nchi kuna changamoto zake. Hapa nitaoredhesha changamoto kubwa ambayo ni "UPATIKANAJI WA WATEJA AU MNUNUZI".
Mnunuzi( Mteja ). Je mtu anafanyaje kupata wateja au mteja katika masoko ya nje. Na nivitu gani mtu anatakiwa azingatie katika kupata mteja wa uwakika na anayeaminika.

Mtaji. Swala la mtaji sio shida maana ukiwa na business plan nzuri inayoshawishi mwekezaji au Bank's huwezi kukosa mtaji. Maana kila mwekezaji lazima ajihakikishie mtaji wake na faida baada ya uwekezaji wake na changamoto nyingine ndogo ndogo ndio awekeze. Biashara kama hii yahitaji uwekezaji katika kufanya tafiti mpaka kufikia hatua yakujirizisha nakuanza kuifanya biashara.

Katika tafiti yangu hii nilibahatika kupata website ambazo zinakutanisha muuzaji na mnunuzi. Website zipo nyingi ila hii link Global B2B Marketplace | Top B2B Trading Platform | TradeWheel hapa ndio niliyoona kidogo ina mambo mengi kwamaana ya bidhaa nyingi zinahitajika au kuuzwa na wauzaji mbalimbali. Ijapokuwa kwa asilimi 50 niliweza kujiridhisha na uhalali wa website hii na asilima 50 zilizobaki nilikuwa na mashaka katika tofuti hii. Pengine tunaweza kupata watu humu waliokwisha itembelea au wako na experience nayo wakatupa mwanga katika hili.

Pascal Mayalla

Naamini katika kujifunza kupitia watu na makosa pia.

Wako mtiifu The Knowledge Seeker

Asanteni
 
Hapa Kuna kitu kizuri.tumezoea kufanya biashara kwa kuagiza bidhaa nje ya nchi sasa ni wakati wetu kuchukua vya kwetu kupeleka duniani..kipindi flani nilizunguka gulf nilistaajabu sana Kuona utitiri wa products za Kenya kwenye mashelve ya shopping mall zao.tena products zao ni zile za kijasiriamali kama za sido tu.
 
Ingependeza kama ungegusia humu bidhaa gani ulizikuta huko ambapo hata tanzania zipo na je unahisi marketing strategy yao wakenya iko vipi ili iwe changamoto kwetu kwalengo lakuisaidia nchi na mwananchi kwa pamoja.

Kutokana na experience yako humo, no bidhaa gani taifa linaweza kupeleka humo.

Lengo hapa nikujua mbinu na kuzijaribu.
 
Kuna kahawa inaitwa Tanica inapatikana Bukoba ni nzuri Sana .

Vijana wengi sio wafanya maamuzi na wengi hawajui kuhusu neno Masoko .

Ila njia bora ni sisi kuwa Marketing strategies na kuhakikisha hatuishii Ku-export raw materials tu bali bidhaa amabazo zimeshaongezewa thamani

Kahawa zinalimwa Bukoba , Kilimanjaro Ila zinaenda Kenya na Uganda na hao Uganda na Kenya wanaziongezea thamani kahawa zao na kuuza ULAYA.
 
Kama zinaenda kenya na kungineko huenda suala la vibali na usafirishaji labda unachukua muda au utaratibu ni mrefu mpaka kuja kupata go ahead ya bidhaa husika.
 
Back
Top Bottom