Swali Lako liko tata kidogo; wataka kujua Kama ni mrefu AMA mfupi kwa wakati huu akiwa na miezi mitatu AMA Kama atakuwa mrefu AMA mfupi hapo baadaye akiwa mtu mzima?
Kama ni kwa wakati huu; tumia chart za ukuaji wa watoto, chart hizi zinapatikana kwenye card za watoto za clinic ambazo zinaonyesha katika kila umri mtoto atakuwa kuwa na urefu na uzito kiasi gani!
Kama ni kwa baadaye ni vigumu AMA haiwezekani kujua kwa Sababu urefu wakati wa utu uzima inakuwaje affected na mambo mengi; generally though Kama wazazi ni warefu mtoto possibly atakuwa mrefu (genetically determined) lakini kuna environmental factors wakati wa ukuaji Kama lishe, maradhi nk vinaweza kumfanya mtu ambaye alikuwa awe mrefu genetically akaishia kuwa mfupi.