Nazikumbuka sana zama zile.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Miaka na zama zilizopita zina raha yake ambayo katu hatuwezi kuipata tena leo.
Gazeti kama Motomoto lilikuwa motomoto kweli, kwani ndilo pekee lililokuwa likiandika habari za vyama pinzani.
Bendi za kipindi kile, Super Matimila, Tancut Almas, Sambulumaa, Washirika Tz Stars a.k.a Watunjatanjata, Marquiz, Mk group, Vijana jazz na nyingine nyingi zilikuwa na ushindani mkali hasa kwenye kinyang'anyiro cha mashibota.
Taarab za kina lssa Matona, Shakila, Bi. Kidude na wengine wengi zilikuwa tamu mno.
Nakumbuka timu za Sigara, Mecco, Pamba na Tukuyu Stars zilivyokuwa zikitamba.
Naikumbuka Nyota Nyekundu ya kina Rosta Ndunguru ilivyokuwa inatembeza daruga.
Nina mengi sana ya kukumbuka ila naomba na wewe uweke unayoyakumbuka.
 
Enzi zile joto la mechi ya Simba na Yanga inapanda mwezi mmoja kabla ya mechi. Siku hizi joto linapanda dakika chache kabla ya mechi
 
Enzi hizo Mbeya kulikuwa na bendi inapiga pale Mbeya Hotel ilikuwa inaitwa Mionzi Band, na sinema tulikuwa tunaangalizia Enterprise Hall opposite na Posta
 
mi nakumbuka redio kaseti na kanda za Mbilia bell
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…