Naziona dalili za Louis Miquissone akitimkia Al Ahly ya Misri

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Salaam.

Kufuatia usajili uliofanywa na Simba SC wa kumchukua winga fundi toka Malawi, Banda, naziona siku za Miq kuendelea kubakia Msimbazi zimefika mwisho.

Tetesi zinasema Simba SC wameshakubali dau la dola milioni moja (Bilioni 2 za kitanzania) toka kwa mabingwa hao wa klabu bingwa Afrika.

Hivyo nikiangalia mlolongo wa matukio, nadhani hiyo ndio sababu iliyowavuta Simba kutoa kiasi kingine cha pesa ili kumsajili Banda toka Malawi, vinginevyo sioni sababu ya Simba SC kumsajili Banda huku tayari wakiwa na Louis Miquissone.

Wana msimbazi tujiandae kusema bye bye kwa mmakonde alieifanyia Simba SC makubwa na kuwa kipenzi cha wana msimbazi.
 
Kiungwana wanatakiwa Wamwachie aende.

Wamtakie mema ni sehemu ya maisha ya soka.

Yeye hatakuwa wa kwanza kuondoka.
mfalme okwi aliondoka na alirudi.
Niyonzima vilevile kwa yanga.

Ikiwa ni kweli akiondoka kwa bilion mbili.hiyo ni right tranfer deal kwa MO.

Akiiacha nitamshangaa.
sasa faida yake hupataga wapi.

Kikubwa simba wamwachilie huyo mchezaji.na wamfanyie Farewell party.
 
Mpira ni maisha yake mchezaji wamuachie akatafute mafanikio mbele ya Safari huko
Kwani yeye mwenyewe anasemaje? Maana kama yeye mwenyewe kachagua kuondoka Simba basi ni busara akapewa nafasi akaangalie maisha mengine na apewe baraka zote kwanzia washabiki mpaka viongozi.
 
Hatuna deni naye.
Mwamba yule

Sent from my LM-V409N using JamiiForums mobile app
Nimeona tofauti hii'Merquison kafanya kazi kubwa anaondoka kwa kuuzwa bei kubwa kwenda Al Ahly,wakati Haruna Niyonzima kafanya kazi kubwa Yanga anaondoka kwa kumwagiwa maji na wenzie siku ya kumuaga pale taifa,hapo ndo mimi niposhangaa.
 
Alie kuambia Miquecon ni mmakonde kakuongopea.
Hivi kwanini wa Tanzania tunaamini kila mmocambique ni mmakonde?

Niwape faida moja, wamakonde ni kabila dogo sana ndani ya Mocambique, kinacho wabeba ni ile wao ndio walio pambana kuikomboa Mocambique kutoka kwa mreno.

Kabila kubwa Mocambique ni Wamakhua.
 
Nimeona tofauti hii'Merquison kafanya kazi kubwa anaondoka kwa kuuzwa bei kubwa kwenda Al Ahly,wakati Haruna Niyonzima kafanya kazi kubwa Yanga anaondoka kwa kumwagiwa maji na wenzie siku ya kumuaga pale taifa,hapo ndo mimi niposhangaa.
Mkuu me sikufichi Yanga imewahi kuwa wachezaji wa kawaida Sana, Yani average Sana kusema ukweli ila walikuwa wanapewa hadhi ambazo hawana, Kwa Ile miaka ambayo Yanga anachukua makombe miaka 3 mfululizo ni Kwa sababu ligi ilikuwa haijawa ngumu kama miaka ya sasa na pia walikuwa wanabebwa kupita kiasi na TFF ndomana hakuna ambalo walikuwa wanafanya wakienda club bingwa

Kwa mchezaji kama haruna niyonzima uwezo wake ule ambao waga anaimbwa kila kukicha sikufichi hajawahi kufikia ata nusu ya uwezo wa laly bwalya huyu aliecheza nusu msimu Tu, alipoenda Simba alimkuta HD wamoto na akakosa namba hebu fikilia Dilunga anamficha niyonzima anaeimbwa ni kiungo bora kucheza vpl? Sikufichi bro Yanga amewahi kuwa na mchezaji nae ni Kamusoko Yule ndio mtu sasa

Niyonzima Alikuwa anaimbwa Sana Ila statistics zinamkataa, haiwezekani kiungo namba 8 Kwa miaka yote ambayo amecheza vpl hajafikisha ata Assist 25 na goli 25, kiungo anaimbwa fundi hakuna msimu amemaliza ata ana assist 6 serious? Sasa huo uzuri wake uko wapi? Kwahiyo bro kusema ukweli Simba ina wachezaji wa level ya juu Sana basi tu watu wanachukulia poa

Yanga hivi sasa ina wachezaji wazuri Sana kuliko Ile miaka ambayo ilikuwa inachukua makombe huo ndio ukweli Ila tatizo linakuja Simba ina wachezaji wazuri Zaid kiasi kwamba wachezaji wa Yanga wanaonekana wa kawaida, laiti kama Simba ingekuwa haichezi vpl Yanga angebeba makombe ata miaka 20 mfululizo Kwa wachezaji alionao,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…