NBA 2016/2017 Season Special Thread

The @washwizards (4-2) advance to the Eastern Conference Semis! [HASHTAG]#NBAPlayoffs[/HASHTAG]
 
Hii inanikumbusha kabla ya mwaka juzi tulikuwa tumezoea kwamba timu yoyote inayomtoa Barcelona kwenye uefa champions league basi ni lazima ichukue ubingwa. Lakini Atletico Madrid Kamtoa barca 2014 alifika fainali na akaambulia kipigo cha 4-1.

Sasa na wewe endelea kujiwekea imani.
 

? Means a lot in that Picture.
 
celtics take 1-0 series lead, defeat washwizards 123-111,
isaiahthomas' 33p, 9a. [HASHTAG]#NBAPlayoffs[/HASHTAG]
 
Leo ndio siku ya last year's eastern conference final rematch.

CAVS VS RAPTOR.

Game tamu sanaa hii kuliko zingine zote.
 
Nina wasiwasi mkubwa na kibarua cha Doc Rivers. Najua timu yao si nzuri kihivyo lakini sikutegemea waondolewe na Utah Jazz.
 



Western Finals; GSW vs Houston Rockets

Eastern Finals; Celtic vs Cavs
 
Sielewi hawa Spurs wamepatwa na masahibu yepi. Maana hii aibu ya leo sikuitegemea kabisa Duh!
 
Sielewi hawa Spurs wamepatwa na masahibu yepi. Maana hii aibu ya leo sikuitegemea kabisa Duh!
Hapana Mkuu, Spurs wamezidiwa tu...hawana ujanja hapa. Mimi nilijua hii game itakuwa ngumu.
 
Reactions: BAK
Nilijua game ni ngumu na ingeweza kwenda either way ila sikutegemea kipigo cha aibu kama hiki tena nyumbani kwa Spurs.

Hapana Mkuu, Spurs wamezidiwa tu...hawana ujanja hapa. Mimi nilijua hii game itakuwa ngumu.
 
Nilijua game ni ngumu na ingeweza kwenda either way ila sikutegemea kipigo cha aibu kama hiki tena nyumbani kwa Spurs.
Ni kweli, hiki ni kipigo cha mbwa mwizi...tena nyumbani! Sijui Pop leo atasemaje! Tofauti ya pts 35+ 108-72 duh!

Update:


Halfway through the 4th Qr the score is 119-82!
 
wat if Spurs tried to play that cavs comeback shit n failed [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hapana Mkuu, Spurs wamezidiwa tu...hawana ujanja hapa. Mimi nilijua hii game itakuwa ngumu.
Spurs watarudi tu game ya pili hiyo sio mara ya kwanza kupoteza game one na bado wakafika fainali kumbuka hata Mara ya mwisho wanachukua ubingwa western conference finals game mbili za kwanza hawakushinda.

Kwa hiyo msiwe na shaka na hicho kipigo hao ndio wanaopambana na warriors kwenye western finals za msimu huu.
Nilijua game ni ngumu na ingeweza kwenda either way ila sikutegemea kipigo cha aibu kama hiki tena nyumbani kwa Spurs.
 
Reactions: BAK

Kiukweli wana kazi sana kuwakaba kina madevu, ubaya wa madevu ni kwamba ukimkaba asi-score jamaa anagawa pasi tu na wenzake hawamwangushi kabisa.

Kwa hiyo inakuwa kazi sana nani wa kumkaba nani wa kumwacha, angalia hata score board wachezaji sita wamepata double digits, si mchezo, lazima waje na plan ya kueleweka.
 
Niliwaambia hapa akina Raimundo huyo Spurs anaweza asikatize mbele ya Rockets na madevu wao wanakasema Pop ni kocha bora sana hawezi kuwaangusha..

Last year hivi hivi masihala masihala OKC akawachapa.. Spurs hawawezi kuifunga timu yeyote yenye offense nzuri mfano wa Rockets na GSW..
 

Sure mkuu, pia nawaona Spurs wako so aged kiasi kwamba hata zile defensive schemes zilizokuwa zinawapa ushindi imekuwa kazi sana kuzitumia kwa sababu ya spidi ya wapinzani.

Nikiikumbuka Spurs iliyoichapa Miami ya kina Lebron 2014, sioni mabadiliko makubwa kwenye kikosi ukilinganisha na timu pinzani. Watu kama kina Parker, Ginobili na P Gasol wanahitaji kupumzika kwa kweli, au wapewe dakika chache sana.

Na changamoto ni kubwa wakikutana na timu ambayo iko offensive minded kama Rockets na GSW, mpaka dakika hii naona kabisa dalili za Cavs kukutana na GSWs finals.
 
teh teh teh nakumbuka kuna jamaa mmoja hapa akasema Spurs imeisumbua sana GSW kwenye regular na wakikutana western finals lazima GSW apigwe..

Ni kweli mkuu, tangia last season mimi nilisema ni ngumu sana kwa Spurs kufunga timu zenye offense nzuri ikiwa wao wanamtegemea zaidi mchezaji mmoja Kawhi na wasaidizi wake akina Parker walikuwa washachoka sana. Mwaka jana pia Tim alikuwa ni mzigo mkubwa sana kwa timu hasa wakikutana na timu zenye offense nzuri na wanaocheza fast basketball.. Spurs wako slow sana hata defense yao sio ile ya misimu miwili iliyopita.. Mwaka wa tatu huu wanamaliza vizuri regular season lakini postseason zinawakataa.. Sasa ni wakati wa kuondoa wazee wote pale wajenge timu upya..
 

Tatizo la Spurs ni Culture yao, kupata wachezaji wanaofit ule mfumo wa Pop ni kazi sana hasa kwa kipindi hiki ambacho watu wanaweka maslahi mbele, ule mkusanyiko wa Parker, Tim na Ginobilli kuweza kukaa pamoja kwa kipindi kirefu vile siyo rahisi kwa kipindi hiki.

Na hata Aldridge hajaweza kabisa kufikia kiwango tulichokitegemea, nadhani wanahitaji kusajili, maana kwa sasa ile mentality ya defense wins inapata changamoto sana.
 
Aldridge alianza vizuri sana, sijui alikuja kukengeuka wapi. Kama angebaki Blazers si ajabu combination ya CJ, Dame na Aldridge na wale role players wao ingewaweka top 4 kwa miaka kadhaa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…