NBA Season 2015 - 2016: Special thread


Game 5 ya OKC na GSW uliingalia?
 
Mkuu ratings zinashuka Warriors ikiwa inashinda pekee teh teh teh.. Ikiwa inashindwa huwa zinapanda. Na sababu labda ni moja tu, NBA sasahivi kuna Warriors Fans and Anti Warriors.. PERIOD..

Cavs walipokuwa wanaidominate Hawks kwa kupiga three pointers 21 alafu wakaja kupiga 25 game inayofuata hakuna shabiki aliyesema hizo game hazimvutii ila ndio kwanza waliipa sifa timu yao.. Sina haja ya kufufua zile tambo wakati Cavs wakigawa dozi kule East..
 
Game 5 ya OKC na GSW uliingalia?
I wish nikupe my twitter account ukaone mwenyewe kwenye timeline yangu nilivyokuwa naiangalia na kutweet wakati hiyo game ikiendelea.. Na labda nikuweke sawa tu maana najua unachataka kukiongea.

Mimi niliaga hapa baada ya loss ya game 3 tukiwa 2-1 nasi sio baada ya kupigwa game 4 na series kwenda 3-1.. Sababu pekee iliyonifanya niage hapa ni ile ile tu kwanza msimu mzima huu nimekuwa nikisema ni OKC pekee ndiyo naiogopa kukutana nayo kwenye postseason na sio Cavs wala Spurs. Game 1 walitupiga lakini niliandika hapa kama game 2 tukirekebisha defense yetu, tukalimit turnovers na tukistep up kwenye offense basi ni rahisi sana kumpiga OKC. Game 2 tulifanya hivyo na nikasema basi OKC tutampiga hizi series.. Tukaja kurudia makosa yale yale ya game 1 wenye Game 3.. Hapo ndio nilikosa kabisa amani ya kushinda hizi series na nikaaga hapa kiroho safi lakini sikuacha hata siku moja kuangalia game zetu.. Game 4 mpaka Game 7 zote nimeziangalia na nilikuwa napita humu kimya kimya hasa game 4 na 5 na kuona jinsi ID zilivyofufuka kuja kushambulia..


And I was a sportsman kwasababu nilivyoaga hapa nilisema wazi kabisa OKC wametuzidi ujanja wala sikuleta visingizio vyovyote vile vingine..
 

Mkuu nimekusoma.

Kwa michezo yote ilivyo, hata timu iwe bora vipi haiwezi kupendwa na kila mmoja, na tena utakuta watu wengi wanainjoy kuona bingwa anafungwa kwa sababu siyo kitu cha kawaida au cha mara kwa mara, hivyo hivyo kwa GSW ya sasa, ikifungwa ndiyo rating zinaongezeka kwa sababu kila mtazamaji anataka kuona jinsi inavyopambana kurudisha.

Ila ikitokea bingwa akawa anashinda kirahisi, kila mtu anapredict matokeo na anaona hakuna sababu ya kupoteza muda kuangalia kitu unachojua matokeo yatakuwaje. Wanaobaki wanaangalia ni wale washabiki hasa wa hizo timu (hasa hasa wa ile timu inayoshinda), neutrals wengi wanapungua.
 
Ni sawa mkuu na ndio maana wewe utabaki kuwa shabiki mwanamichezo kwa wale Anti Warriors hapa.. Labda kidogo na huyu mchagahalisi ingawa yeye wengi tunamwona kama Comedian hapa teh teh teh..

Tulivyoshinda hizi game wewe umekuwa muwazi kwamba Cavs wamekukatisha tamaa na Warriors imestahili lakini wengine kabla hata ya kuipa credit timu pinzani wao wanakimbilia kutoa maneno ambao yako nje ya mchezo. Na ndio maana kwenye post yangu moja hapa nilisema hatuongelei basketball tena watu wanaanza kuongelea ratings..

Swahiba wangu BAK alikuwa anachekelea sana Warriors walivyokuwa wananyanyaswa na OKC kwenye game 3 na 4 na series kwenda 3-1 wala hakusema Series hizo hazimvutii kuangalia teh teh teh
 

Mkuu hakuna mahali niliposema wamenikatisha tamaa in terms ya series nzima, nimesema hawajacheza vizuri game 1 na 2 ila siyo kukata tamaa kabisa.

Bado nafasi tunayo, 2 bila siyo gap kubwa if your team have a King.
 
"The Cleveland Cavaliers' chance to win this series is zero as far as I'm concerned." - Stephen A. Smith
 
"The Cleveland Cavaliers' chance to win this series is zero as far as I'm concerned." - Stephen A. Smith
teh teh teh Stephen alinichekesha sana ile game 2 ikiwa inaendelea alivyosema leo anataka kuichana Cleveland game likiisha na liwalo na liwe ila ataichana sana tu...
 
Ni hapo ndipo naukubali msimamo wa Nyani Ngabu msimu huu, alikiri toka awali kabisa kuwa GSW ni timu ngumu na hivyo hata akidai fainali imekosa msisimko namuelewa...msimu huu hajawahi kuiponda GSW!

Nisiowaelewa ni wale ambao pamoja na CAVS kutandikwa kwa pointi 34 mwezi wa Januari, waliendelea kuisifu wakidai safari hii GSW watakiona na kwamba msimu uliopita walibahatisha tu kwa CAVS kuwa na majeruhi.

Nakumbuka walivyosema kuwa mathalan katoka Platt na kuingia Lue, GSW wasitegemee mteremko! Sasa watu hao hao leo kudai kwamba fainali haina msisimko kwa sababu tu tayari GSW kamtandika CAVS 2-0! Hakika siwaelewi.

Cha kushangaza ni nini? Kwani wakati CAVS wanaisulubu Pistons, wanawasulubu Hawks, wanawasulubu Raptors je hawakujua kwamba mbio za CAVs mwisho ni kwa GSW? Kwamba kwa GSW msimu huu, CAVS wako 0-7!

Pamoja na kwamba Steph Curry ni shabiki wa GSW kama mimi na sikubaliani naye 100% kwa mengine lakini kwa hili yuko sawa. Wako watu hawaipendi GSW kiasi cha kutokuwa tayari kukiri uwezo mkubwa walio nao kimchezo.
 
Nimekuelewa,Bruv!
 
Stephen A Smith yupo so close to the Cavs. And he said tangu regular season Inaelekea ukingoni kuwa The Cavs want Golden State Warriors so badly and i can't wait for the series to happen. Hata wakati warriors went down 1-3 against the OKC jamaa alisema I hate the Not to see the Warriors against Cavs coz Cavs were ready for the Warriors. So lazima awe disappointed with how the series have turn out to be.
 
Pamoja na kwamba Steph Curry ni shabiki wa GSW kama mimi na sikubaliani naye 100% kwa mengine lakini kwa hili yuko sawa. Wako watu hawaipendi GSW kiasi cha kutokuwa tayari kukiri uwezo mkubwa walio nao kimchezo.

Kwa nini unilazimishe kukiri ubora wa timu ambao mimi sijaukubali? Ubora uko subjective, unachokiona bora wewe siyo lazima na mimi nikione ni bora.

Pia kwa nini tulazimishane kushabikia timu moja? Kuna kuongoza darasani kwa sababu darasa lina vilaza tupu, na ndicho ninachokiona kwa sasa GSW anachofaidika nacho. Ni wa kawaida sana.

Kama ni mshabiki wa mpira utakumbuka kuna kama misimu miwili Barca alidominate sana Spain, kabla Mourinho hajaenda kule, kwa washabiki wa Barca ilikuwa safi sana, lakini kwa neutrals ligi ilipunguza mvuto kwa sababu unakuwa unajua bingwa ni nani.
 
Naona wengine mnachukulia michango yangu too seriously ha ha haa! I am only enjoying myself...ukitaka kuniona nikiwa serious ingia uwanja wa siasa inayoaffect maisha yangu. Huko mtu anahitaji siyo seriousness tu bali na uvumilivu kwani akina Jesca wako wengi wakiishi na kusoma kwa pesa zetu kumbe ni vilaza. Poleni mlioumia.
 

Ha ha ha, haiumizi hii. Kikawaida kwenye huu ushabiki bana ukiona unazidiwa unajificha, maana hakuna atakayeenda kukufichua huko na kukwambia uje hapa, ukiona tuko hapa ujue tunainjoi game, iwe tumefungwa au tumefunga, ushabiki ni zaidi ya matokeo ya game moja au mbili au hata series.
 
Baada ya tafakuri nzito naomba nichukue nafasi hii kuwaaga wapenzi wote wa jukwaa hili na hasa mchezo huu wa Basketball. Huu utakuwa ni mchango wangu wa mwisho baada ya kubaini nawakwaza wachangiaji wengi kwa kutumia maneno yanayoonekana yanawaudhi baadhi yenu. Lengo langu wakati wote ni, pamoja na kuchokoza mjadala, kujadili mambo kwa namna ya satire kupunguza stress baada ya mihangaiko mitaani. Wakati wote sina nia mbaya kwa yeyote na nawatakia kila la heri na may the best Basketball team win this season. Pamoja na kwamba mimi ni mwanamichezo through and through, nitaendelea kusoma lakini sitachangia tena...asanteni kwa uvumilivu pale nilipopitiliza utani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…