NBC hatari kwa wateja wake

Igabiro

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
242
Reaction score
27
Nimepigwa pesa katika benki ya NBC , Jmosi niliweka kama 1.7m tawi la NBC DODOMA, kwenda kuchukua pesa benki jtatu nikakuta nimepigwa 1.5m kupitia NBC tawi la Tegata kwa kutumia ATM card yangu ambayo ninayo mwenyewe, cha ajabu mie nko DOM na pesa imepigwa DSM, Nawashauri ndugu zangu wenye account NBC wacheki account zao
 
NBC kitengo cha mawasiliano ni wezi, siwaamini kabisa. Ulipowauliza hapo NBC wamesemaje mkuu?
 
Duh hii ni hatari sana,pole sana mkuu ila usisite kufuatilia kwa ukaribu watakurudishia tu kilicho chako
Ngoja wazee wa vibubu tuendeleze mila
 
Wanasema niandike barua then nifuatilie, but kuna watu kama watano nao wamepigwa Dar es Salaam na nasikia kwenye camera anaonekana ni mzungu ndiye anayefanya mchezo huo
 
Asante kwa taarifa mkuu ngoja tuchukue tahadhari
 
Duh!Sasa hapo kosa ni la nani? Si inatakiwa hela yako urudishiwe au? Mbona watatuumiza wengi aisee kwa mtindo huo?
 
Tatizo tunalalamika hatuchukui hatua kwani hii sio mara ya kwanza kuona post ya mtu kupigwa kazi ya benki ni kutunza pesa na kkama pesa zinapotea zikiwa chini ya benki wanapaswa kukurudishi kama utafunguia kesi kwenye mahakama ya biashara NBC watazuiwa kufanya biashara ya benki popote duniani mabenki mengine kama Backrays yana insurance na issue kama hiyo ikitokea wanakulipa na wao wanaendelea kushugurika(kutafuta wapi makosa yamefanyika) we wanakwambia andika barua ya nini tayari wamepoteza sifa yao kama benki inabidi tuamke vinginevyo kila siku tutakuwa tunalalamika.
Mimi nina akaunti NBC siifungi nawangojea waje wafanye huo mchezo
 
kupigwa maana yake nini? anyway wapo waliokuelewa,
 
Ela yangu ninavyoifutailia wakiikwapua tuu ninao
Toa mihera yako weka bank zingine au tigopesa au mpesa maana unaweza lia kama mtoto unapokuwa unataka ela kwa account haimo
 
Komaa nao hao mpaka wakurudishie hela zako, ukilegeza inakula kwako. 1.5m haiwezi kupotea hivi hivi tu.
 
Benki ya NBc imesha poteza mwelekeo wa kihuduma wafanyakazi wanaopokea mishahara yao kupitia benki ya nbc hucheleweshewa hadi mwanzo wa mwezi mwingine
 
Ndugu habarini? Kama kuna yoyote anatumia nbc nashauri akacheki balance kuna unusual transactions, watu wengi pesa zimechotwa mpk staff
chukueni hatua haraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…