NBC kuwa bank bora Tanzania na nje ya Tanzania

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
6,782
Reaction score
12,716
Ndugu wa Tanzania nimekuwa nikifuwatilia kwa ukaribu vile bank hii vile inatoa huduma zake pamoja na bidhaa zake kwakweli mwenye macho haambiwi tazama, huu niwakati wa watanzania kujuwa kule tunaenda ktk uchumi wa Tanzania basi kuikosa hii bank nikujikosesha fursa ktk maisha yako. NBC Ltd wamejizatiti katika kulinda amana za wa Tanzania katika kutoa huduma bora tena za kimataifa. Uwez kuamini nchi za magharibi, ulaya na asia wanaitambuwa hii bank kias mara nyingi wawapo Tanzania wanaziaminia Atm za Nbc pamoja na huduma zao. Hakuna mtu alie patwa na tatizo ktk wiz wa kwenye mtandao hajapata pesa zake baada ya uchunguz hili limeifanya bank hii ya wa Tanzania kuwa angaza wa tz popote walipo. Serikali inaujuwa mchango wa hii bank na ndio maana haijawah tangaza kuachia sehem ya hisa zake kwa wa wekezaji, pia kama ulikuwa hujuwi sasa hivi hii bank inamfumo wa kisasa ambao unahifadhi mafail ya wateja kiasi kupotea taarifa za mteja ni kama hadithi sasa. Huduma za mobile bank, ebanking vimeboreshwa kiasi sasa kweli maisha kiganjani na sio tena siri kwamba ukitaka kitu lazima uchukue physical casha, hudua ya e statement inaenda punguza habari yakuja bank uchukue statement. Bank ktk upande wa matumizi ndio ucguse kabisa imejipanga kwa ku2mia low fuel cars jambo linapunguza matumizi, huduma zote ktk electronic kupunguza paper work. Nizaidi yaku make yani huwez kuifananisha nbc na bank nyingine kwa vile imetoka analog nakwenda digital!
 
Jingle...waambie walete bank master yao bongo kwanza
 
....wamenifurahisha kwa ile application yao kwenye play store , I can view my account kupitia smartphone yangu...
 
Jana serikali imetoa ruksa kwa benki mbili hapa nchini kutoa huduma za kibenki kwa akaunti zote za serikali na wafanyakazi wa serikali sasa ruksa kufungua akaunti na kuhudumiwa na benki yoyote kati ya NMB na CRDB BANK. Hivyo halmashauri zote nchini zinatakiwa kuchagua benki ipi itahudumia katika halmashauri husika mapema wiki ijayo.
[/IMG]
Mimi natoa pongezi kwa benki hizi mbili na hii ni nafasi yenu sasa kuonyesha mko vizuri kuhudumia serikali na wafanyakazi kwa ufanisi. Fungua kiambatanisho cha barua kwa maelezo zaidi
 
Hamna benki nzuri kama kibubu. Kibubu chanitosha
 
Hamna benki nzuri kama kibubu. Kibubu chanitosha

NBC imenunuliwa na Barclays na zote huo uboreshaji wa Huduma ni wa Barclays ambayo ni benki ya mapepari kwa hiyo hazitaki Wateja wadogo wa kibiashara. Ndiyo maana hawataki kujiandikisha kwenye soko la hisa hapa nchini. Benki nzuri ni NMB na CRDB tu.
 
NBC imenunuliwa na Barclays na zote huo uboreshaji wa Huduma ni wa Barclays ambayo ni benki ya mapepari kwa hiyo hazitaki Wateja wadogo wa kibiashara. Ndiyo maana hawataki kujiandikisha kwenye soko la hisa hapa nchini. Benki nzuri ni NMB na CRDB tu.

Sina hakika sana ila nafahamu kuwa tokea mwanzo NBC ılimilikiwa na ABSA ya South Afrıca ambao walikuwa majority shareholder, kampunı ambayo pia ilimılıkı bank za Barclays Africa.Sasa wamebadili jina lao na wanajulikana Barclays Afrrican Group.Bank zao kuna wakatı ziliyumba hadi wakafanya retrenchment kubwa sana, ila sasa wanarudı.Mzungu anajua kuchanganya karata achana naye.Hao CRDB mtawasıkıa, NBC inakuja.
 
NBC hiihii ninayo ifahamu au NBC ipi?

Aisee Kama ndiyo msemaji wao umekuja kuiuza nenda waambie wadekebishe uozo wao uliojaa matawini.... Mtu utafikiri uliwalazimisha ku-bank nao bwana au pesa ni zao
 
NBC imenunuliwa na Barclays na zote huo uboreshaji wa Huduma ni wa Barclays ambayo ni benki ya mapepari kwa hiyo hazitaki Wateja wadogo wa kibiashara. Ndiyo maana hawataki kujiandikisha kwenye soko la hisa hapa nchini. Benki nzuri ni NMB na CRDB tu.

na posta bank
 
Mabenk yote na mifuko ya hifadhi za jamii,kwa Tanzania yapo kihuni huni sana wanatumia udhaifu wa serekali yetu hi ya kijani kuwanyonya watu mpaka basi.
 


Pinda @Work
ni ukichaaa kwa Serekali yenye HISA NMB kupeleka Biashara benki Nyingine Binafsi.
 
Mtoa hoja unaishi ulaya nn? NBC ndio bank inayoongoza kutojali wateja, nenda kwenye branch utaona kwakuanzia tembelea tegeta branch kwa dar,
 
NBC kitengo cha internet banking kipo hovyo sana, yaani unaenda kuomba service ya online banking, huyo mtu unayeelekezwa kwake hajui A wala B. Unaenda kuongea nae say unamuomba maelekezo kuwa unahitaji security code zilizotumwa toka Paypal, anaanza kukushangaa, haelewi hata hiyo paypal ni kitu gani.

Nimeenda kuomba service ya online banking mpaka leo danadana hakuna jibu linaloeleweka. No wonder hao wezi waliowapiga pesa hawakutumia akili nyingi sana.

Ukija service toka kwa wahudumu wake ni tabu tupu, hawajali wateja, dharau kibao na mengi ya kukera.
 
NBC ni uozo haswaa. Binafsi nimeshaibiwa kwenye akaunti yangu mara kadhaa, ukienda kutoa malalamiko wanakuambia ukae siku 45 ndo watashughulikia. Hiyo Mobile Banking nimeomba toka Januari 2015 nikaambiwa ndani ya wiki moja itakuwa tayari mpaka leo 5/4/2015 sijapata majibu. Tellers ndo uozo zaidi wabibiii wazeee wamechokaaaa
 

Mkuu we January 2015?? Me toka July Kama si August last year (2014) na kubandika mapicha na kujaza mafomu lakini waapiii?? Nikakumbushia Mara mbili holaaa....nikaona nipotezee tu niendelee ku-enjoy na Simbanking tu

Isingekuwa taasisi ninayofanyia wanatumia NBC na akaunti ningeshaifunga kitambo
 
Cathode Rays hao NBC kwa kweli ni janga, kuna mtu aliniambia kuna kosa lilifanyika wakati Fulani watu walikuwa wanajiri/ kupandishwa vyeo (esp. BRANCH MANAGERS) bila kuangalia WELEDI, TAALUMA na UZOEFU sasa ndo matokeo yake haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…