Wapendwa wana JF: Naamini nyote mnakumbuka utaratibu n amatangazo ya kuboresha taarifa za kibenki kwa wale wenye akaunti zao. Naomba kuwakumbusha tangazo la NBC, pamoja na maelezo mengine benki hii ilieleza kuwa wanaostahili kuboresha taarifa ni wale ambao waliofungua akaunti kabla ya Julai 2007.
Mimi ni mmoja wa wateja wa benki taja na nilifungua akaunti October 2007 katika tawi la Industrial area,
Cha ajabu tangu mwezi uliopita benki inagoma kunipatia huduma kwani kila niendapo ATM mashine naambiwa "No transaction permitted", baada ya kuingia kaunta kwa wahudumu wamenijulisha kuwa sikuboresha taarifa za kibenki na kwakuwa nilifungua tawi nikiwa shule nikafungua kama mwanachuo, inanipasa kwasasa kuboresha taarifa eti anuani zangu za sasa ni tofauti. Maswali ya kujiuliza ni mengi, mfano;

- Mimi mteja wao ninakosa gani?
- Kwanini tangazo lao halikueleza wanaotakiwa kuboresha kwa makundi yao?
- Ninani atakaye lipa gharama hizi na usumbufu ninaoupata kwasasa?
- kwanini kitengo chao cha mahusiano na jamii kisiwajibishwe kwa kuninyanyasa mtanzania