Zamani niliifunga account yangu Benki ya Posta kwa sababu ukitaka kuweka au kuchukua pesa yako kule uombe ED kabisa kazini, maana siku nzima itapotea kwa kwenda kuweka au kuchukua 10,000/= Tena mahali pengine hata kama balance yako ni milioni 10 watakwambia mwisho kuchukua ni 10,000/= ati hawana hela ya kutosha. Nikaishiana nao kwa kuniudhi walipokaa na kitabu changu miezi 8 eti wanapiga hesabu ya faida waniingizie kwenye kitabu. Nilipofuatilia nikakuta mtu mmoja makao yao makuu kakiweka kitabu changu kwenye draw yake akidai bado anakifanyia kazin(Baada ya miezi 8).
Nikaona NBC bora. Lakini nao wakaaza kuboa taratibu na hatimaye mb** wao ni mkukwa zaidi. unaenda na kadi yako counter yenye picha yako kabisa na saini kwa nyuma. Kwyenye system wanaiona balance yako. Wanakusainisha nyuma na mbele kwenye karatasi zao za kuchukulia pesa, lakini bado wanataka upitie ATM kuuliza salio ambako wanakata 75/=, Ukikosea ukarudia tena unakatwa tena. Ukichukua pesa wanakata 500/= ukichukuwa mara mbili kukamilisha 600,000/= wanakata 1000/= wanakuuliza unataka huduma nyingine? ukikubali ukasema labda niulize swali wanakata. Hawaweki faida (Interest) kwenye pesa yako, kila mwisho wa mwezi wanakata tena ati ni ledger maintenance fee. Wizi---wizi---wizi!
Halafu counter zaweza kuwapo 6, lakini utakuta kuna mhudumu 1 au wawili tu, quee ni ndeeeeefu lakini hawajali, unakuta wanapiga story ndani na wengine wanajipitishapitisha wakikata viuno kwenye vyumba kutoka chumba kimoja hadi kingine, halafu wanaingia kwa vyumba vya wahudumu walioko counter na kuanza kuwasemesha story na kupeleka kazi za ndugu zao za kuwawekea na au kuwachukulia pesa ati hawawezi kupanga mstari. Sasa NBC wanataka kufanana na Benki ya Posta.
NMB nao ndio SACCOS hasa! Wao wanakata viuno kwenye makorido wakijipitishapitisha wakati wateja wamejaa hata wanashindwa kupumua bali wanapumuliana. Kama una wivu na mkeo na umekwenda naye utakufa kihoro kwa namna wanavyombana kwenye msitari. Hata konokono anayo speed kubwa wanavyofanya kazi. ATM wameanza kuweka na hawakati pesa, lakini zinaweza kuwapo 2 ukakuta ama mbovu zote au moja tu inafanya kazi, watu hujaa mno, maana chini ya laki tano ati lazima uende ATM. Halafu Kadi zao kumbe zinaexpire bwana. yaani weacha tu.
Sio hapo tu lakini, ukienda Muhimbili hospitali kwa mfano, ati wanataka mambo mapya ya kisasa, computerised services kila kitu. Nguvu ya savor ni kaduchu na wao wanataka mambo makubwa. Mteja mmoja kumwandikisha alipe akamwone daktari ni nusu saa au zaidi, wanadai mtandao uko slow leo. Unaweza kuamua kupona hapohapo kabla ya kumwona huyo daktari wao. Hata akikuona daktari, anakwambia kalipie vitu hivyo.... unakwenda kukaa tena kwenye mstari weeeeee! Kwa nini tunaanza system ambazo hatuziwezi?
Na nyie BoT mko wapi wezi wa mabenki wanatamba tu nanyi mmelala? Au nako tupeleke EWURA?