NBC: Wizi wa kutumia kitechnologia

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
Kwenu wana JF,

Kwa siku mbili nimewasikia wafanyakazi wenzangu wakilalamika kwamba wameenda kuchukua pesa katka ATM za NBC na kukuta pesa zao zote zimechukuliwa na watu wasiofahamika.Wameripo Benk na inaonekana wahusika wanatoa ushirikiano LAKINI wanaongea na walalamikaji faragha ili jambo hili lisiwafikie wateja wengine.Kwa wale mulio na taarifa za kina naomba mtuambie ni TECHNOLOGIA gani inatumika katika huu wizi na tufanye nini tusiibiwe???

Nawasilisha.
 
kuna jamaa wamemlamba over 4M NBC wanatumia ATM ..... statement inaonyesha siyo yeye na wamechukua within 3 days
 
Wizi wa kupitia ATM upo almost every bank ndani ya Tanzania, wanaohusishwa na wizi huu nasikia ni wa bulgaria, wakenya pamoja na wazungu wa kutoka marekani. Unaweza kupata habari zaidi ya aina ya wizi huu hata kwa kutumia google search engine. Nakushauri fanya hivo kwa faida yako na jinsi gani ya kujilinda kama mteja.
 
Naanza kupata picha ya huu wizi.Nasubiri mawazo zaidi.Nawakilisha
 
Je, Technologia waliotumia NBC katika kuandaa Master card zao ndiyo dhaifu kiasi cha kusasababisha huo wizi kwa wateja wake kadhaa ???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…