darcity
JF-Expert Member
- Jul 20, 2009
- 9,101
- 18,055
Leo ni siku ya USAILI kwa watu walioomba nafasi za ajira za ukarani wa sensa itakayofanyika tarehe 23 Agosti 2022. Nilichoshuhudia ni uwepo wa dosari katika mbinu ya kuwapata watakaopewa ajira ya muda katika zoezi hilo. USAILI kwa njia ya mdomo na walioteuliwa kufanya usaili.
Wasimamizi wa maudhui walioteuliwa ambao pia ndio wanaosaili waomba kazi ni baadhi ya wakuu wa shule za msingi na sekondari. Hawa wasaili tayari wana watu wao ambao pia ni waombaji. Ikumbukwe nao waliomba ikaja bahati wakateuliwa katika nafasi za usimamizi maidhui. Wapo wenye wake zao,watoto zao,shemeji zao lakini pia kuna wafanyakazi wenzao wenye migogoro nao.
Pili ni njia usaili wa mdomo. Hii ni maarufu na inayotumika sana kupata waajiriwa. Ni nyepesi lakini pia inapima uwezo wa ufahamu wa muajiriwa,mwonekano pamoja na tabia zake kulingana na mahitaji ya muajiri. Ilichofeli NBS ni kutumia maswali hayo hayo kwa waomba ajira zaidi ya laki tano nchi nzima! Time interval na idadi chache ya wasaili hairuhusu maswali hayo kutovuja/inatoa mwanya maswali kuvuja.
Toka saa tatu asubuhi, maswali yameshazagaa mitandaoni! (Ikiwemo humu Jamii forums) na kutoa nafasi kwa waliochelewa kufanyiwa usaili kuyajua na kutafuta majibu. Kama watatumia hayo maswali Kama kigezo kikuu basi wafaidika ni wale wa mwisho kufanyiwa usaili. Naamini NBS watarekebisho hizo kasoro ama siyo zoezi la sensa litaenda kuharibika na kutia taifa hasara ya mabilioni.