Naamini ukibaki msomaji wa kawaida kama mimi hupungukiwi na kitu ,ona sasa tutataka kujua uwezo wako wa kufikiri na kiwango chako Cha Elimu.
Naomba nikujibu kwa uelewa wa wengi na utaniambia kama hujaridhika.
Kwanza tambua sensa ni Rais na Rais ni sensa, zoezi hili toka mwanzo msimamizi Mkuu ni Rais kwa Sababu taarifa za maswali ya sensa yatamsaidia Rais kutekeleza majukumu yake ipasavyo na ni Rais ndio anatakiwa kuwataka, kuwaomba na kuwasihi watu washiriki zoezi Hilo.
Hapo aangaliwi mtu maarufu kwa Sababu hata kingwendu ni maarufu kuliko Anna Makinda ,hapo kinachoangaliwa ni nani mwenye uhitaji wa taarifa za sensa kati ya Anna Makinda na Rais Samia?. Jibu ni Rais Samia, kama ndivyo basi ni yeye ndio kuwaomba watu taarifa hizo.
Mtazamo wangu
Yawezekana mtazamo wangu usiwe sahihi lakini una ukweli ndani yake, zoezi hili Upinzani wanaona kama ni moja ya siasa za CCM. Mtanzamo huo unafanya wapinzani wengi washindwe kushiriki zoezi hili muhimu kwa kujua au kutokujua.
Uhalisia
Uhalisia wa zoezi hili ni kwamba sensa ni mkakati wa maendeleo kwa watu hivyo Rais kuwa mstari wa mbele kukuhamasisha ni kwa nafasi aliyonayo katika maendeleo ya nchi yetu. Rais Kama mdau namba moja wa maendeleo ni lazima aone umuhimu wa kila mtu kushiriki