NCAA - Utaratibu wa malipo Ngorongoro unahitaji maboresho!

NCAA - Utaratibu wa malipo Ngorongoro unahitaji maboresho!

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Hapa naongelea kivutio cha NGorongoro
Naona kuna usumbufu usio wa lazima ambao unaweza kupatiwa ufumbuzi kama mamlaka wataamua kufuata ushauri wa wadau wanao waletea wageni

1. Mgeni akibadilisha tarehe ya kuingia Ngorongoro hata kwa siku moja, kwa sababu zozote zile
Haruhusiwi kuingia hadi atume email kwa mamlaka ndio abadilishiwe tarehe. Cha ajabu ni kuwa hakuna anayetuma akataliwe sasa, kwa nini system isiruhusu kubadili tarehe angalau kwa siku moja au mbili? Hii ni kero kwani ndege zinabadilika kila siku na unajua tena efficiency ya system zetu, hii inahitaji ujibiwe email kwa haraka sana ili upange safari; lakini je mabadiliko yakitokea usiku (ndege nyingi huja jioni/usiku), Jumapili, sikukuu? nk, Lakini pia, ni kwa nini waongeze kazi isiyokuwa na ulazima hasa kwa kipindi hiki? system inaweza kuwapa report ya changes zooote.
Nimeandika nikijua kuongezeka au kupungua kwa magari 12- 20hivi kwa siku hakuna impact kubwa

2. Permit hulipiwa kwa masaa 24, sasa Mfano, unakuta wageni wanaingia saa tatu, kesho yake wanatoka saa sita; Tatizo la system yao ni kuwa hairuhusu mtu alipie siku moja + Entry
Badala yake una ambiwa mwendesha wageni akisha ingia ndani ya hifadhi ndio uongeza day?
Yaani wanaongeza kazi zisizo kuwa na lazima kwa kitu cha kurekebisha tu kwenye system lndani ya muda mfupi!! si wanao ma IT tena wabobezi?

3. Pendekezo
Nafikiri kwa geti zao mbili ambazo ndio malango makuu; Loduare na Nabi
Wangefunga Camera kama zile za traffic kwa ajili ya kusign out permit (hakuna haja ya kupanga foleni gari likitoka park)
Kwa mtu ambaye permit yake iko poa, inapiga picha gari na ndio anakuwa amesha sign out anaondoka;
Kwa yule permit ina overstay inapiga alarm anaenda kulipia. Kwa namna hiyo msongamano kwa mageti ungepungua kwa kama 40%
Sasa hivi kila kitu manual; mtu wa getini au guide akijisahau, unashangaa baada ya siku kadhaa una ambiwa gari linachajiwa kila siku eti bado lipo ndani
 
Umeongea kitu cha msingi sana mkuu mimi nimeingia huku Mwaka huu nilikua nafanya hii kazi SA naona vitu vingi vinafanyika kienyeji kama vile NCCA hawahusiani na Utalii wa wageni ukiwashangaa nao wanakushangaa wao mpaka nikauliza huku Tanzania ipo kweli bodi ya Utalii na je pana Chama cha Tour Operator ambao wanajitambua kwenye hii kazi mbona vitu vingi haviwafanyi wageni kurudi tena unakuta mgeni kachoka eti mnapanga pale Foleni niliwahi ulizwa tunapanga foleni ya nini hapa nilivyowajibu wageni walishangaa sana wakasema kwa hiyo hii foleni ni kila siku ipo na nyinyi mnaona sawa tuu...
 
BODI INAENDESHWA NA WASHAMBA AKILI MGANDO.KAZI KUPEANA NA KURISISHANA KINDUGU.HAMNA KITU PALE NI MAZEZETA NDYO WANAENDESHA BODI NAKULIPIANA POSHO KUBWA
 
Pana madereva wengine pale Getini wanapita tuu adhabu anaipata aliechukua Permit hasa kwa muda mwingine unaotumia gari za kukodi...pale wameferi kupita maelezo Kruger unapita unavyoingia unapita unavyotoka kwenye mbuga pana vioo vimewekwa karibu na geti la kutokea ukigonga mnyama au mnyama akiegemea gari attacha alama wakiwa na mashaka na wewe ndio utakaguliwa Getini ila sio kwa vibali vya Park Serikali inachaji USD ila haitaki itumike kwa kitu chochote ili kuboresha na kupunguza kadhia kwa wageni ili wafanye kurudi tena...
 
Umeongea kitu cha msingi sana mkuu mimi nimeingia huku Mwaka huu nilikua nafanya hii kazi SA naona vitu vingi vinafanyika kienyeji kama vile NCCA hawahusiani na Utalii wa wageni ukiwashangaa nao wanakushangaa wao mpaka nikauliza huku Tanzania ipo kweli bodi ya Utalii na je pana Chama cha Tour Operator ambao wanajitambua kwenye hii kazi mbona vitu vingi haviwafanyi wageni kurudi tena unakuta mgeni kachoka eti mnapanga pale Foleni niliwahi ulizwa tunapanga foleni ya nini hapa nilivyowajibu walishangaa sana...
Huku kwetu wasomi wazuri kwenye Wizara ila sijui tatizo ni nini?
Mf: Mgeni akitaka kibali cha kupiga picha pamoja na kuwa tayari kulipia malipo yote
Hakuna mtu mwenye Mandeti na hicho kibali, nenda huku, nenda kule hadi unakata tamaa au upate Kishoka
 
Huku kwetu wasomi wazuri kwenye Wizara ila sijui tatizo ni nini?
Mf: Mgeni akitaka kibali cha kupiga picha pamoja na kuwa tayari kulipia malipo yote
Hakuna mtu mwenye Mandeti na hicho kibali, nenda huku, nenda kule hadi unakata tamaa au upate Kishoka
Usomi mzuri sio vyeti mkuu usomi ni vile unavyoona hilo eneo limeboreshwa hilo ndio lango la Wageni mimi binafsi vingi nashangaa kwa kuwa ukiuliza hiki unaambiwa nenda kule muda mwingine unafatilia vibali ukiwa na Wageni hasa hivyo vya Picha sasa kwa nini hawarahisishi wakati wenzao malipo ya kupiga picha ni kidogo tuu tena unaomba online ukilipia ilikua kama Camera huna unaandika Camera na Lens unayotaka hivyo vitu utakutana navyo getini hii Corona ilivyoisha Makampuni ya Utalii yalipewa favour kuingiza watalii mbugani karibu miezi mitatu bure kabisa haulipii chochote...Makampuni makubwa Tanzania ndio yana taarifa ya kila kitu vitu vingi vya utalii havipo wazi vina password..
 
Ni hivi hii NCHI sehem Muhimu zimejazwa VILAZA. Watu wakishapokea hela za Mishahara tyr wamelizika na Maisha. Hawana focus, Creativity, Hawana Uchungu.
 
Back
Top Bottom