Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi amesema wale vijana wadogo kwenye Siasa wanaodhani watairudisha nchi hii kwenye mfumo wa chama kimoja wanajidanganya na kuota ndoto za mchana.
Mbatia amesema alifukuzwa Chuo Kikuu pale UDSM tarehe 10/02/1992 siku ya Jumatatu kwa sababu ya harakati zake za kupigania mfumo wa vyama vingi. Anadai aliporwa haki yake ya elimu hali iliyomlazimu kupata elimu ughaibuni huko Uholanzi.
Naye Wakili Joshua amesema mfumo wa chama kimoja ni ugaidi kwani watu hutafuta haki zao kwa kutumia mapanga na marungu.
Mhhhh! Wanasiasa hamna tofauti na Yuda eskalioti wengi wapo kwa ajili ya matumbo yao tu na si kingine mwanasiasa wa kibongo hana tofauti na ile jinsia nyingine yenye tamaa