Uchaguzi 2020 NCCR-Mageuzi kufanya uzinduzi wa kampeni Septemba 5, 2020

Uchaguzi 2020 NCCR-Mageuzi kufanya uzinduzi wa kampeni Septemba 5, 2020

NCCR Mageuzi

Member
Joined
Oct 3, 2007
Posts
23
Reaction score
63
Hayawi hayawi, sasa yamekuwa, ni rasmi sasa chama cha NCCR-Mageuzi kimejipanga kufanya uzinduzi mkubwa wa kampeni zake za uchaguzi Septemba 05, 2020 kwenye viwanja vya Zhakeim, Mbagala Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Uenezi na Mahusiano ya Umma ndugu Edward Julius Simbeye amesema chama kimejipanga kufanya kampeni tofauti na zile wanazofanya vyama vingine vya siasa huku akiita ni uzinduzi wa kampeni ya Kisayansi ambayo itaenda kumnadi mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Yeremia Kulwa Maganja pamoja na chama kwa ujumla.

Kwenye uzinduzi wa Kampeni pia chama kimepanga kuzidua rasmi Ilani ya chama.

Untitled-1.png
 
Kila la heri
Mje na suluhusho la changamoto za hali ya uchumi na ukosefu wa ajira
 
Hongereni sana!
Promo iwe ya kutosha nyumba kwa nyumba ..
Kama tunavyowategemea next KUB
 
Back
Top Bottom