NCCR - Mageuzi, mguu sawa yajipanga tena baada ya miaka 30 ya Mageuzi

NCCR - Mageuzi, mguu sawa yajipanga tena baada ya miaka 30 ya Mageuzi

Dr Shekilango

Senior Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
192
Reaction score
120
Ni wazi chama cha NCCR-Mageuzi kinajipanga kufanya kazi kubwa katika siasa za Tanzania baada ya miaka 30 ya Mageuzi ya kisiasa Tanzania. NCCR-Mageuzi ni mwasisi wa siasa za vyama vingi na Mabadiliko ya katiba mpya, wao wanajita THE SUPER OLD PARTY (SOP)

Taarifa za ndani ya chama hicho zinadokeza chama hicho kinajiandaa na matukio mawili ya kukihuisha chama hicho moja linatarajiwa kufanyika mwezi huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee eneo kilipozaliwa miongo mitatu iliyopita na lingine litafanyika mwaka kesho, hii yote ni kuendelea kujiimalisha katika siasa za Mageuzi.

Baada ya uchaguzi chama hiki kilijifanyia baadhi ya mabadiliko kadhaa ikiwa ni pamoja na kuanzisha KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAARIFA, mwanzo hakikuwa mfumo huo. Mabadiliko mengi yamefanyika hasa baada ya uchaguzi, na sasa chama hicho kinajianda kufanya siasa za uongozi na kuwa mbadala au serikali kivuli. "Kuna mambo makubwa yanakuja kwenye chama chetu alisikika mmoja ya kiongozi kijana na mwenye ushawishi ndani ya chama hicho, tegeni masikio mwezi huu kila mtu atakubali upinzani kurudi kwenye asili yake".


THE SUPER OLD PARTY (SOP)


FB_IMG_1633544703528.jpg
 
Waingie mchezoni tu maana Chadema ishajifia tuone mageuzi kamili ya James Mbatia
Aaahahaaaa Eti chadema ishajifia HII HII ambayo hata wakipita wanatembea wamevaa nguo zao wanakamatwa au nyingine.

Daaah nmecheka Sana aisee eti chadema ishajifia watu WA CCM bhana wakati mwingine mi huwa nawaonea huruma Sana aisee
 
Kumbe NCCR nao ni "demokrasia na maendeleo"!.
 
Ccm B wanajiimarisha vipi wakati wapo kwenye line?
 
Kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2020 mlliwapamba kuwa watakuwa na wabunge wengi na mkafika sehemu mkawaambia kuna majimbo 20 ya free, naona mmerejea tena !
 
NCCR ni chama kilichojaa wasomi, tofauti na Chadema iliyojaa wanywa viloba, wavuta ngada, wauza gongo na wapiga kabali za mbao.
Ok sawa kingekuwa kimejifia wqla usingesikia mtunkakkita hapa maana thread ni ya nccr lakini CDM inatajwa
 
NCCR ni chama kilichojaa wasomi, tofauti na Chadema iliyojaa wanywa viloba, wavuta ngada, wauza gongo na wapiga kabali za mbao.
Yaani CCM mlivyo waoga mkisikia hata wanawake tuu wa Chadema wanafanya mazoezi mnaanza kujamba na kujiharishia.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom