Chama cha NCCR-Mageuzi tunapenda kuweka msisitizo wa taarifa tuliyoitoa tarehe 16 Januari 2021 katika kikao chetu cha halmashauri kuu ya Taifa. Taarifa inayohusu Ugonjwa wa Virusi vya Korona-19 (UVIKO-19).
NCCR-Mageuzi tunawaomba watanzania kuongeza mbinu za kujikinga kwa kiwango kisichopungua 70% ikiwemo kuzingatia taratibu zilizowekwa za kujikinga na ugonjwa huu bila ya kukosa ambazo ni;
- Kuvaa barakoa
- Kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia sabuni na maji tiririka
- kutumia vitakasa mikono
- kuzingatia umbali uliowekwa kitaalam kati ya mtu na mtu
- kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima
- kuepuka msongo wa mawazo
- Na tahadhari bunifu nyingine zenye kuokoa ugonjwa huu
Kadhalika, NCCR-Mageuzi inaungana na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kupitia waraka wa Rais wake Mhashamu Baba Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga wa tarehe 26 Januari 2021 kuhusu UVIKO.
Kuhusu waraka wa TEC, Soma Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini