Kesi nyingine ni ya Jimbo la Kawe ambapo wanaamini kuwa maneno ya Nkya kwamba mgombea wa chama hicho, James Mbatia ananyanyasa wanawake yalisababisha wanawake na wasichana kuwapigia kuwa wanawake wenzao.
Aliwataja wanawake hao kuwa ni Mdee aliyeshinda na Angela Kizigha wa CCM aliyeshika nafasi ya pili.
Alisema sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985, inakataza kushawishi kupiga kura kwa kufuata jinsia, na shauri lingine linamtaka Mdee kuthibitisha kauli yake kwamba Mbatia kapewa milioni 80 na CCM kutokana na kutokuwepo na hesabu za kupokea kiasi hicho cha fedha
katika vitabu vya hesabu vya vyama hivyo.
"Kwa misingi hii, Halima Mdee alijua kuwa anasema uongo, basi alikusudia kupotosha
wapigakura na kama aliyasema yana ukweli atakuwa amevisaidia vyama hivyo juu ya ufujaji mkubwa wa mali za vyama na njia ya kujua kweli ni kufika mahakamani," alisema.
Alisisitiza kuwa kesi ya Mdee na Nkya ni ya uchaguzi lakini wanaweza kufunguliwa kesi
nyingine na Mbatia kudai bilioni moja kwa kumdhalilisha kutokana na kutoomba msamaha katika siku walizopewa.
Hata hivyo, Nkya alishasema kuwa alinukuliwa vibaya na gazeti (si Habarileo) wakati Mdee alikanusha kuwa hajawahi kusema mambo hayo
Huyu jamaa kwan ni wa jinsia gani? Mbona ana mabifu na wanawake? Kwanini asimshataki na huyo wa CCM?