Poleni ndugu zangu,
Ni kwamba Daniel Nsanzugwanko mbunge aliyepita alikuwa mwanachama wa NCCR Mageuzi mwaka 1995, alitumia resource nyingi kukijenga chama huko na alikubalika sana na inadhaniwa alishinda katika uchaguzi ule akachakachuliwa live, baada ya hapo akajisalimisha CCM badala ya kuendelea kujenga upinzani dhabiti, mwaka 2005 alirudi kugombea baada ya kifo cha mbunge wa jimbo hilo.
Kwa kuwa watu walifikiri bado ana mawazo ya kuleta maendeleo walimwamini tena, kumbe alikuwa ameshabadilika na hakufanya lolote la kujivunia Kasulu, wakati wa kampeni alikuwa mkali kama pilipili kwa watu waliokuwa wakiuliza maswali ya kutaka kujua alifanya nini au kwa nini alihama NCCR mageuzi, kosa alilofanya kubwa ni kupiga watu vibao kwenye mikutano ya hadhara eti ni vibaraka wa upinzania wakati yeye alikuwa huko.
Hivyo NCCR Mageuzi ina nguvu sana huko sababu ya Mheshimiwa Nzanzugwanko kuweka misingi imara, siyo Kasulu na Kibondo bali hata Kigoma Ujiji mwasisi wa mageuzi huko na Dr.Aman Walidi Kabour aliyefanya Chadema ikubalike mpaka leo unawaona akina zito na wengine ni matunda ya akina Kabuor.
Kivuli chake ndiyo kimemwangusha Bwana Nsanzugwanko, siyo majimbo hayo tu Kasulu magharibi napo CCM iliponea chupuchupu kwa tofauti ya kura 4.