Elections 2010 NCCR Mageuzi wameniduwaza...


Mkuu Keil,

Lakini mbona hiyo haikutokea sehemu mbalimbali? Kwa mfano najua yule jamaa wa CHADEMA kule Mbeya vijijini ni mzuri sana na ni kiongozi wa CHADEMA wa mkoa na pia muda mwingi kajichimbia kule Mbeya lakini bado hakuweza kushinda. Kuna majimbo mengine pia ambayo kuna vijana ambao walipiga kampeni za nguvu lakini hawakufanikiwa.

Hii ya Kigoma naona kama ni pekee kwa siasa za Tanzania mwaka huu. Huenda kujijenga kwa hao vijana wakiwa ndani ya CHADEMA kumewasaidia maana tayari walikuwa wanajulikana lakini pia kuna hao wengine wawili ambao nao wameshinda.

Kama kuna mtu anajua matokeo ya udiwani kwenye hizo wilaya ingesaidia.

Kigoma Mjini CHADEMA alikuwa anagombea bwana mdogo mmoja ambaye tumesoma naye nchi moja. Nilisikitika kuona alishindwa dakika za mwisho tena kwa kura chache sana zenye utata. Nafikiri angelikuwa na muda wa kutosha wa kujijenga kule kama wenzake huenda angeshinda kwa kura nyingi.
 

Poti,

Kunatofauti ya kushindwa kwa kura au kushindwa kwa kuiba kura. Wewe poti nakupa pole kwa sababu walichakachua kura zako ila hawa ninao waabudu wameshindwa kwa kura. Sitasahau pale mgombea mmoja alipomaliza kuongea na watu wakaanza kutawanyika na kuwaacha wangombea wengine wakishangaa du hii ndiyo demokrasia.

Naona watu wamekujibu la NCCR lakini na mimi bado sijapata majibu ni kwa nini Kyela walikuwa wanampenda dr vile na kuwafanya muonekane vile wanajamii wenzetu!
 
Ukweli ni kwamba Samweli Ruhuza tajiri mkubwa na katibu wa NCCR-Mageuzi ni mwenyeji wa Kigoma. Huyu jamaa ameishi Kigoma muda mrefu na anafahamu watu gani wangefaa na mahali gani. Ukiondoa David Kafulila wengine wote wametokana haswa na juhudi za Samweli Ruhuza wala sio kina Mbatia.
 

Mkuu Shalom,
Kule kwetu Kyela kuna matatizo makubwa mno ya umaskini na ujinga. Badala ya kushambulia kila post yangu hapa JF, utakuwa umetimiza wajibu wako kama mwana Kyela na Mtanzania ukitumia hata dakika chache kuangalia namna ya kupambana na hayo matatizo.

Nani anapendwa zaidi ya mwingine haitakusaidia maana siasa ndivyo zilivyo miaka yote. Si umeona kuna wagombea wamejaza watu mpaka pa kukaa pakakosekana na bado kura hazikutosha? Kura kama 1600 nilizopata tena bila kuchakachua au kumwaga makadi feki zinanitosha na ninasonga mbele na life yangu. Kama unaona ni chache basi kajaribu na wewe tuone.

Tuache kupotezeana muda hapa JF bila sababu za msingi. Kuna mambo mengi ya kufanya zaidi ya politics.
 
K. amanda uliyotangulia mwanzoni, kweli unafahamu kilichojiri Kigoma...kama lilivyojina langu Zitto anajifanya ndio kingmaker wa Kigoma na alikisaliti chama na kuwapigia kampeni hao mentee wake wazi wazi. Alimrubuni Mzee wa watu Ntagazwa kuhamia chadema na amekuwa akimpiga chenga kwenda kufungua kampeni zake. Hata Dr. Slaa alipoenda hakwenda hata kuzungumza nae na Dr. Slaa alimwambia arudi kutibu majeraha na kuona kwanini Ntagazwa hakubaliki na Zitto wala hakurudi. Yeye alikuwa tayari kwenda Mtwara kupigia wanachadema wengine lakini mkoani kwake ambako amwekea mapandikizi wake hakukanyaga mguu..sitoshangaa akikosa kuwa Kiongozi wa Upinzani bungeni na masuala mengine akaanzisha chama chake au akaenda huko NCCR...what goes around comes around...
 
Kamanda uliyotangulia mwanzoni, kweli unafahamu kilichojiri Kigoma...kama lilivyojina langu Zitto anajifanya ndio kingmaker wa Kigoma na alikisaliti chama na kuwapigia kampeni hao mentee wake wazi wazi. Alimrubuni Mzee wa watu Ntagazwa kuhamia chadema na amekuwa akimpiga chenga kwenda kufungua kampeni zake. Hata Dr. Slaa alipoenda hakwenda hata kuzungumza nae na Dr. Slaa alimwambia arudi kutibu majeraha na kuona kwanini Ntagazwa hakubaliki na Zitto wala hakurudi. Yeye alikuwa tayari kwenda Mtwara kupigia wanachadema wengine lakini mkoani kwake ambako amwekea mapandikizi wake hakukanyaga mguu..sitoshangaa akikosa kuwa Kiongozi wa Upinzani bungeni na masuala mengine akaanzisha chama chake au akaenda huko NCCR...what goes around comes around...

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…