Habarindiyohiyo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 263
- 16
Wakati huo huo, mwandishi wetu Hilary Komba, anaripoti kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi ya NCCR-Mageuzi, Bw. Faustin Sungura, alisema wahariri hawakupaswa kuandamana bila kwanza kujiridhisha iwapo habari iliyosababisha gazeti kufungiwa ilifuata maadili ya kitaaluma na kwamba ilikuwa ya kweli.
"Maandamano ya wahariri hayakutakiwa kufanyika kabla ya kufanyika uchunguzi wa kina, kwa sababu kwa sasa kuna baadhi ya watu wamejitokeza wanataka kulishitaki gazeti hilo sasa kama litaonekana lina hatia mahakamani basi wahariri watajiweka katika nafasi mbaya," alisema Bw Sungura.
Kwa maoni yake, alisema wahariri wameharakisha kuandamana kabla hata ya kufanya uchunguzi kwani inaweza kuwashushia hadhi yao, ambayo ni muhimu katika Taifa ambalo linawahitaji kwa kazi zao.
Alisema wahariri wana haki ya kuandamana kama haki zao zikiwa zimekiukwa kama kufungiwa magazeti, lakini wanapaswa kufahamu kuwa jambo wanalodai lazima liwe limefanyiwa kazi kwanza.
Aliongeza kuwa iwapo ingebainishwa kwanza ukweli wa habari hiyo, hata chama chake kingekuwa tayari kushirikiana kwa karibu zaidi kupinga hatua iliyochukuliwa ya kulifungia gazeti la MwanaHALISI.
Nacho Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiliunga mkono maandamano hayo katika ilichokiita salamu zake za mshikamano kwa wanahabari nchini zilizotolewa jana na Mkurugenzi wa Vijana wa Chama hicho, Bw. John Mnyika.
"Tunawapongeza wahariri kwa mshikamano wenu katika kipindi hiki cha majaribu; endeleeni kusimama pamoja, ni umoja wenu ndio utakaokuwa kinga ya pamoja dhidi ya mtu au chombo chochote kinachoingilia uhuru wenu.
"Mshikamano wenu ni ishara ya kushindwa kwa mkakati wa wagawe uwatawale na imani kwamba umoja ni nguvu. Wahariri wote hawapaswi kukaa kimya kuhusu kufungiwa kwa MwanaHALISI, kwa kuwa leo ni kwa gazeti hilo, kesho itakuwa kwa gazeti lingine; hivyo ni vyema kuungana kulinda uhuru, taaluma na sekta ya habari," alisema.
Chama hicho kililaumu jinsi hatua hizo zilivyochukuliwa kwa kusema ni sawa na Serikali kuamua kesi ambayo yenyewe ndiyo ilikuwa imelalamika.
"Hatua ya Waziri mwenye dhamana na sekta ya habari kugeuka mlalamikaji, mwendesha mashitaka na mfungaji ni mwelekeo mbovu wa kupuuza taasisi za kusimamia uwajibikaji na haki.
"Uamuzi uliofanywa na Serikali hauna tofauti na unaofanywa na raia wanaojichukulia sheria mikononi(mob justice).
"Kwa Serikali inayoheshimu misingi ya asili ya haki, tulitarajia chombo chochote cha habari, kikivunja sheria ama kukiuka maadili dhidi ya serikali, viongozi wake ama watu binafsi mashitaka au malalamiko yangepelekwa kwa taasisi zinazohusika mathalani Baraza la Habari (MCT) au Mahakama," aliongeza.
Chanzo: Udokozi toka MAJIRA