Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza cha Ugonjwa wa UVIKO19 katika jimbo la Wuhan nchini China, maambukizi ya virusi hivyo yamepindukia visa milioni 200 huku zaidi ya watu milioni 4.5 wakipoteza maisha. Kubadilika kwa aina za virusi vya corona kama Alpha, Beta, Delta nk., kunaongeza chumvi kwenye kidonda cha maafa yanayosababishwa na virusi hivyo.
Mataifa mengi yamechukua hatua za kudhibiti kuongezeka kwa virusi vya corona kwa njia mbalimbali ikiwamo kuweka katazo la kutoka nje, kufunga viwanja vya ndege, kutoa chanjo nk. Katika baadhi ya nchi, njia hizi zimeonekana kuzaa matunda, na sasa nchi hizo hazina tena maambukizi ya virusi vya corona.
Zifuatazo ni nchi zilizotangaza kutokuwa na maambukizi ya virusi vya corona duniani.
15. Visiwa vya Solomon
Taifa hili lenye visiwa vikubwa 6 na mamia ya visiwa vidogo Mashariki ya Visiwa vya Vanuatu limeshuhudia visa 20 tu vya maambukizi bila kifo chochote cha mgonjwa wa corona. Kwa sasa, wagonjwa wote walioripotiwa wamepona na taifa hilo halina tena maambukizi mapya.
14. Visiwa vya Marshall
Taifa hili liliripoti visa 4 vya UVIKO19 mwezi Oktoba mwaka 2020, ambapo wagonjwa wote walipona. Tangu wakati huo, visiwa hivyo vya Bahari ya Pasifiki havijaripoti visa vipya vya maambukizi.
13. Vanuatu
Taifa hili la Visiwa vya Kusini mwa Bahari ya Pasifiki imeripoti visa vitatu tu vya maambukizi tangu kuzuka kwa maambukizi ya UVIKO19, bila mtu yeyote kufariki. Kituo cha Kukabiliana na Magonjwa cha Marekani kinaonya watu kutosafiri kwenda visiwani humo kutokana na wasiwasi wa kutokuwepo takwimu sahihi za hali ya maambukizi visiwani humo.
12. Tuvalu
Taifa hili lenye jumla ya visiwa tisa vikiwa na ukubwa wa kilometa 26 za mraba lipo katikati ya Hawaii na Australia lina wakazi zaidi ya 10,000. Hatua za mapema za kujilinda zimesaidia nchi hii kutopata maambukizi ya virusi vya corona, na sasa limefanikiwa kutoa chanjo kwa wakazi 10,861.
11. Turkmenistan
Nchi hii ipo katikati mwa Bara la Asia ni moja kati ya mataifa ambayo hayajaripoti kuwa na maambukizi ya virusi vya corona mpaka sasa. Taifa hilo, hata hivyo, linachukua tahadhari zote za kujilinda zikiwamo kuzuia mikusanyiko, kufunga safari za kimataifa na limetoa chanjo kwa zaidi ya wakazi 41,000.
10. Tonga
Taifa hilo lenye visiwa 36 vinavyokaliwa na watu kati ya visiwa 170, limefanikiwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona kwa kuzuia meli kuingia katika fukwe zake mwanzoni mwa mlipuko, pamoja na kuweka katazo la kutokutoka nje kwa taifa zima. Zaidi ya watu 73,600 wamepatiwa chanjo kati ya watu 100,000 kufikia mwezi Septemba.
9. Tokelau
Ingawa linatambulika kama taifa, Visiwa vya Tokelau vinategemea New Zealand kwa kiasi kikubwa. Udhibiti wa maambukizi kwa wakazi 1,500 umefanikiwa kwa 100%, huku watu 968 wakipatiwa chanjo kufikia Agosti 2, 2021.
8. Saint Helena
Hili ni eneo la nje la Uingereza, na linatajwa kuwa visiwa vilivyo mbali zaidi na nchi kavu kuliko visiwa vyote duniani, vikiwa umbali wa zaidi ya kilomita 4,000 kutoka pwani ya Brazil na kilometa 1900 kutoka pwani ya Kusini mwa Afrika. Visiwa hivi havijaripoti maambukizi wala vifo vinavyotokana na UVIKO19.
7. Visiwa vya Pitcairn
Visiwa hivi vilivyo katika Bahari ya Pasifiki vinatajwa kuwa moja ya mataifa yenye watu wachache zaidi duniani, vikiwa na chini ya wakazi wa kudumu 50 tu. Licha ya kutokuwa na kisa chochote cha maambukizi, watu 73 waliokuwepo visiwani humo wamepatiwa chanjo ya UVIKO19 kufikia Julai 21, 2021.
6. Korea Kaskazini
Hili ni taifa pekee kubwa duniani kuripoti kutokuwa na maambukizi ya UVOKO19 mpaka sasa. Ukweli wa Korea Kaskazini kutokuwa na maambukizi unatiliwa shaka kutokana na historia ya usiri wa taifa hilo la kikomunisti duniani. Taifa hilo lenye wakazi milioni 25 halina rekodi ya visa vya maambukizi, vifo wala idadi ya watu waliopata chanjo.
5. Niue
Visiwa hivi vilivyopo takriban kilomita 2,400 kaskazini mwa New Zealand vimefanikiwa kuhakikisha havina kisa chochote cha maambukizi, huku vikisaidiwa kwa kiasi kikubwa na taifa la New Zealand kutoa chanjo kwa zaidi ya watu 2,300.
4. Nauru
Moja kati ya mataifa madogo zaidi duniani, likiwa na kisiwa kimoja tu lenye ukubwa wa kilometa za mraba 20 tu, limeweza kudhibiti maambukizi kwa kuzuia muingiliano na mataifa jirani, huku likitoa chanjo kwa zaidi ya watu 14,000.
3. Kiribati
Moja kati ya mataifa maskini zaidi duniani, likiwa na visiwa zaidi ya 33 vilivyotapakaa pande zote za mstari wa Ikweta, taifa hili limefanikiwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona kwa kuzuia muingiliano kutoka mataifa jirani.
2. Visiwa vya Micronesia
Taifa hili linaundwa na zaidi ya visiwa 600, likiwa na eneo lenye ukubwa wa jumla ya kilomita 778 za mraba. Licha ya kutoripoti kisa chochote cha maambukizi, Marekani, China na Japan vimetoa msaada kwa Visiwa hivyo kukabiliana na mlipuko wa corona.
1. Visiwa vya Cook
Taifa hili lenye visiwa 15 kwenye Bahari ya Pasifiki Kaskazini mwa New Zealand limefanikiwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona kwa kuweka ulazima wa kukaa karantini wakati wa kuingia na kuzuia meli za abiria kuingia. Tayari watu 21,700 wamepatiwa chanjo kufikia Agosti 2, 2021.