Nchi 188 zathibitisha kuwa na Corona Virus

Nchi 188 zathibitisha kuwa na Corona Virus

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mlipuko wa ugonjwa wa #COVID19 ulianza Desemba, 2019 mjini Wuhan China. Hadi hivi sasa ugonjwa huo umeenea kwenye nchi na mataifa 188

Vifo zaidi ya 470,795 vimeripotiwa kataika jumla ya maambukizi milioni 9.05 yaliyoripotiwa dunia nzima. Huku watu milioni 4.8 wakiripotiwa kupona

Hadi hivi sasa Taifa la Marekani linaongoza kwa kuwa na maambukizi mengi zaidi ikifuatiwa na Brazil
 
Huku mtaani kwetu mpaka tumeanza kusahau hilo neno "corona", tulishaishinda vita yake kwa ushindi mkubwa sana. 😅😅

Asante sana JIWE!
 
Hayo mataifa yanashindwaje kuja Tanzania kufundishwa namna ya kumuomba Mungu? Lakini pia Magufuli ametufundisha kuwa usipotangaza maambukizi na waliokufa corona inaisha yenyewe
 
Hayo mataifa yanashindwaje kuja Tanzania kufundishwa namna ya kumuomba Mungu? Lakini pia Magufuli ametufundisha kuwa usipotangaza maambukizi na waliokufa corona inaisha yenyewe
Corona inaishi vichwani mwetu tu
 
Mmm!, kumekosekana mada au ndiyo leo umefaham corona imeingia?
 
Corona sio shida Africa,labda uwe na matatizo mengine.
Ndugu zetu Kenya wataendeleza usanii hadi lini?
 
Tz ndio nchi ya kwanza kufungua shule baada ya corona sisi wabishi........
 
Pamoja na US kuongoza kuwa na vifo na maambukizi mengi lkn cha ajabu,watu wameeandamana wiki tatu mfululizo bila barakoa wala social distance,juzi Trump kaanza kampeni zake kwenye ukumbi uliokuwa na watu zaidi ya 6200 ,watu hawa kuzingatia social distance na wala barakoa.

Hapo ndio utagundua maisha ya kila siku lazima ya endelee,US yenyewe mpaka sasa najiuliza LOCKDOWN IMEISHIA WAPI ? au wanaharakati wale wa kusisitiza lockdown nao wapo wapi? na yule balozi wa US TZ nae alimwandikia waraka Trump kufanya mkutano bila kuzingatia kanuni za kujilinda na barakoa?

MWISHO WA SIKU MAISHA LAZIMA YA ENDELEE HAIJALISHI INCHI NGAPI ZIMEKUMBWA NA CORONA.
 
Back
Top Bottom