Nchi 9 Zashiriki Tamasha la 43 la Bagamoyo

Nchi 9 Zashiriki Tamasha la 43 la Bagamoyo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

NCHI 9 ZASHIRIKI TAMASHA LA 43 LA BAGAMOYO

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa Tamasha la 43 la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo limeshirikisha Nchi 9 Duniani pia limetoa fursa za ajira na biashara kwa wananchi wa Bagamoyo na washiriki wa Tamasha hilo.

Mhe. Dkt Ndumbaro ameyasema hayo wakati akizindua rasmi Tamasha la 43 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Oktoba 23, 2024 ambapo amezitaja mingoni mwa nchi ambazo zimeshawasili ni pamoja na Comoro, Africa ya Kusini na Zambia, ambapo nchi zingine zitawasili leo.

Mhe. Dkt Ndumbaro amesema Tamasha hilo linatoa fursa kwa wakazi wa Bagamoyo ambao wataweza kufanya biashara pamoja na kuonyesha bidhaa zao ili waweze kunufaika kiuchumi.

Katika hatua nyingine Dkt. Ndumbaro ameagiza Tamasha hilo kufanyika kwa siku 7 kuanzia mwakani badala ya siku 4 kama ambavyo limefanyika sasa lengo likiwa ni kuendelea kutoa fursa ya kuitangaza Bagamoyo na Nchi kwa ujumla katika nyanja za kijamii, kiuchumi pia kujitangaza Kimataifa
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-10-24 at 14.39.05.mp4
    10.7 MB
Back
Top Bottom