Nchi gani ya Ulaya ina visa rahisi?

Nchi gani ya Ulaya ina visa rahisi?

Khalid91

Member
Joined
Feb 2, 2020
Posts
61
Reaction score
43
Wakuu habari,

Ni nchi gani ya Europe ambayo mtanzania akitaka kwenda kwa matembezi mafupi visa yake haina gharama kubwa sana. Nyingi naona zinahitaji insurance ambayo ni euro 30000 ambayo ni kubwa sana.

Tusaidiane wenye experience.
 
Ni insurance ya nini kubwa hivyo? na wao wakija huku kwetu tuna walipisha Insurance kubwa hivyo?

Kuna haja ya sisi ku copy kila kitu kwao, waki tu-charge insurance Euro 30,000 nasi tunafanya hivyo kwao, wakiitoa nasi tunatoa, hii kufanyana wajinga inatosha sasa.
 
Wakuu habari,
Ni nchi gani ya Europe ambayo mtanzania akitaka kwenda kwa matembezi mafupi visa yake haina gharama kubwa sana. Nyingi naona zinahitaji insurance ambayo ni euro 30000 ambayo ni kubwa sana.
Tusaidiane wenye experience.
Mkuu hakuna insurance yeyote kwa pesa hizo euros 30000 ,,
Nadhani umechanganya na insurance covered ,,
Insurance ya ulaya na inchi za shengen na UK ..
zipo inchi 51 utaweza kwenda kwa insurance moja.
Kuanzia euro 15 kwa siku.
Euros 30 kwa week..
Inategemea na kampuni ya insurance..
Na validity ya hyo insurance yenyewe..
Hyo 30000 ni thamani ya hyo insurance yako wewe msafiri incase umepata tatizo. ,,
wanaweza kukugharamia kwa pesa hizo..hiyo sio insurance ya kuilipia pale ubalozini msafiri,,
wewe hupaswi kulipa hiyo,,
Hyo ni thamani ya insurance tu.,kama ukipata tatizo lolote utatibiwa kwa gharama hizo,,30,000,ambazo ni za kwao sio zako.
Sababu insurance zinatofautiana ,,,zipo hadi 180,000, zipo 150,000 ,,
Maana yake ukipata tatizo utatibiwa kwa pesa zisizozidi hizo,,
Na hyo 30000 euros ndy insurance yenye thamani ya chini kabisa,,
Ukiwa na pesa unakata hizo kubwa..
 
Na ktk inchi ulaya yenye viza rahisi ,
- ulaya yote ina vigezo vinavyofanana,,ktk uhitaji wa viza..
Kuna kipindi ubalozi fulani wanatoa viza kwa kipindi fulani ,,
Wakati balozi zingine wanakuwa wagumu kutoa viza.
Baadae hawatoi,,hata uwe na vigezo gani..na zile balozi ngumu viza zikatoka.
Baada ya inchi fulani kulegeza masharti,,watu wanapata viza,,
Mradi tu..usichoke kujaribu..na uwe kamili..
Kwa kifupi inategemea na siku wameamka vipi.
Kuna siku nilishalipia viza balozi wa Italy,
Nikasubiri viza processing hadi jioni,,wakasema njoo kesho ufate viza yako..
Kwenda kesho viza cancelled..
Sijuwi kulitokea nn?
 
Mkuu hakuna insurance yeyote kwa pesa hizo euros 30000 ,,
Nadhani umechanganya na insurance covered ,,
Insurance ya ulaya na shengen na UK zote ni moja..zipo inchi 51 utaweza kwenda kwa insurance moja.
Kuanzia euro 15 kwa siku.
Euros 30 kwa week..
Inategemea na kampuni ya insurance..
Na validity ya hyo insurance yenyewe..
Hyo 30000 ni thamani ya hyo insurance yako wewe msafiri incase umepata tatizo. ,,
wanaweza kukugharamia kwa pesa hizo..hiyo sio insurance ya kuilipia pale ubalozini msafiri,,
wewe hupaswi kulipa hiyo,,
Hyo ni thamani ya insurance tu.,kama ukipata tatizo lolote utatibiwa kwa gharama hizo,,30,000,ambazo ni za kwao sio zako.
Sababu insurance zinatofautiana ,,,zipo hadi 180,000, zipo 150,000 ,,
Maana yake ukipata tatizo utatibiwa kwa pesa zisizozidi hizo,,
Na hyo 30000 euros ndy insurance yenye thamani ya chini kabisa,,
Ukiwa na pesa unakata hizo kubwa..
Mkuu sijakuelewa tafadhali.... yaani wanakutibu kwa euro zisizozidi 30,000 hali ya kuwa umelipia euro pungufu au. Tafadhali sijakuelewa
 
Nina maana hyo insurance yako thamani yake ni euros 30000.
Si zaidi ya hapo.
Hata hapa Tz insurance zina kiwango cha matibabu,,,
Unapolipa kiasi fulani utatibiwa kwa gharama zisizozidi kiasi fulani
 
Nina maana hyo insurance yako thamani yake ni euros 30000.
Si zaidi ya hapo.
Hata hapa Tz insurance zina kiwango cha matibabu,,,
Unapolipa kiasi fulani utatibiwa kwa gharama zisizozidi kiasi fulani
Ook yaani likitokea la kutokea inaweza kukuhudumia mpaka euro 30,000
 
Ook yaani likitokea la kutokea inaweza kukuhudumia mpaka euro 30,000
Yaa..
Ndy maana kuna aina za insurance unazotakiwa kulipia wakati wa kuomba viza..
Mfano zipo insurance kwa siku euros 15..
Utalipia kwa siku utakazokaa..
Na insurance ina expired date..mfano umekata insurance tarehe 10/10/2020..
kuanzia siku utakayoingia ulaya ndy siku inaanza kufanya kazi..hadi siku zile ulizoomba kuishi kule ziishe.
Ukikaa siku nyingi kuliko insurance maana yake haitofanya kazi tena.
 
Back
Top Bottom