SoC04 Nchi haiwezi kuwa na maendeleo pasipokuwa na miundombinu rafiki kwa wananchi wake

SoC04 Nchi haiwezi kuwa na maendeleo pasipokuwa na miundombinu rafiki kwa wananchi wake

Tanzania Tuitakayo competition threads

Hmp mpili

New Member
Joined
Jul 14, 2023
Posts
1
Reaction score
0
Kama ilivyo ada neno miundombinu haliwezi kuwa geni sana kwenye maskio ya watu. Miundombinu ni zile rasilimali ambazo zinapatikana nchini kwa lengo la kuwasaidia wananchi katika kaisha yao.

Mfano wa miundombinu ni kama barabara, shule, vituo vya afya nk. Ningependa kueleza ni kwa namna gani hatuna budi kuliza miundombinu ambazo zinazotuzunguka kwani inchi haiwezi kuwa na maendeleo pasipokuwa na miundombinu rafiki kwa wananchi wake.

Naweza kuchukulia mfano daraja la mkapa. Ni moja kati ya kiunganishi kikubwa sana kwa watu wa mikoa ya kusini na kaskazini. Mfano katika kipindi hiki cha mvua za elimino zinazoendelea kunyesha kwa wingi hadi kusababisha uharibifu katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.

Kwa watu wa rufiji naweza kusema tunaipongeza sana serikali yetu ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kutujengea daraja la mkapa kwani kwasasa linawasaidia walio wengi kufanikisha malengo yao. Kwa kushirikiana na vyombo vya usalama sisi kama wananchi tunapaswa kuwa walinzi na watunzaji wazuri wa miundombinu hii kwani itawasaidia kizazi na kizazi.

Hivyo basi hiyo ni moja kati ya miundombinu tunazopaswa kuzilinda na kuacha kuharibu. Vituo vya afya pia vinamchango mkubwa kwenye maisha yetu hivyo tunapaswa kuvitunza.

Kupitia serikali yetu tukufu imejitahidi sana kuhenga vituo vingi vya afya nchini kwa lengo la kusaidia wananchi wake. Kutokana na hali hiyo naomba nitoe rai kwa wananchi wenzqngu tunapaswa kuwa mabalozi wazuri kukemea yale yote yanayolenga kuharibu miundombinu za inchi yetu.

Kwani inchi haiwezi kuwa maendeleo pasipokuwa na miundombinu zilizokuwa bora. Mfano mzuri kwenye nchi zilizoendelea kama Uingereza, China, Marekani. Hizo ni kati ya inchi ambazo zina miundombinu bora na ndio maana zinamaendeleo makubwa.
 
Upvote 2
Kwani inchi haiwezi kuwa maendeleo pasipokuwa na miundombinu zilizokuwa bora. Mfano mzuri kwenye nchi zilizoendelea kama Uingereza, China, Marekani. Hizo ni kati ya inchi ambazo zina miundombinu bora na ndio maana zinamaendeleo makubwa.
Ahsante kwa kuliona hilo na hii haswa ndiyo kazi ya serikali.

Kimsingi serikali ni kufanyia kazi miradi na miundombinu ya kimkakati kwa ajili yetu wanaserikali wenyewe. Natamani kila mmoja alione hili. Ahsante
 
Back
Top Bottom