Nchi hii kumbe madaktari feki wapo?

Brightman Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2009
Posts
1,224
Reaction score
234
Tumekuwa tukisikia bidhaa feki, trafiki feki, ARV feki, madawa feki. Jamani watz nani atatuokoa na majanga haya? Ebu soma feki nyingine hii hapa chini:

KCMC yamnasa daktari feki akiandaa upasuaji
Na Rehema Matowo
Posted Alhamisi,Septemba5 2013 saa 20:27 PM
Kwa ufupi
Alikuwa wodi ya watoto akitaka kumfanyia upasuaji wa ngozi mmoja wa wagonjwabaada ya kuomba rushwa ya Sh200,000.

Moshi. Taharuki na hofu imewakumba wagonjwa waliolazwa katika Hospitali yaRufaa ya KCMC ya Mkoa wa Kilimanjaro, baada ya uongoziwa hospitali hiyo kumkamata daktari feki aliyekuwa na nia ya kumfanyia upasuaji wa ngozi, mmoja wa wagonjwa aliyekuwa hospitalini hapo na kutapeliwa Sh200,000
Alikamatwa katika wodi ya upasuaji akijinadi kwamba ni daktari wa watoto ametambuliwa kuwa ni Alex Sumni Massawe, ambaye alikamatwa jana asubuhi na makachero wa Polisi waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia baada ya uongozi wa hospitali hiyo kumuwekea mtego.
Kabla ya kukamatwa kwa Massawe, Mama mzazi wa kijana aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji wa ngozi, PamvelinaShirima alikutana na daktari huyo katika baa moja maarufu mjini hapa (jina limehifadhiwa) na kumtaka ampatie Sh200,000 ambazo atazitumia kuharakisha mwanae Makasi Tipesa afanyiwe vipimo .
Ofisa Uhusiano wa Hospitali hiyo,Gabriel Chisseo aliwaambia waandishi wa habari kwamba Massawe aliwekewa mtego na uongozi wa Hospitali ya KCMC kutokana na baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na daktari huyo feki. Alisema mama wa mgonjwa alipewa taarifa na rafiki yake kuwa anaweza kumpatia daktari atakayemsaidia kupata huduma kwa haraka,ambapo alimkutanisha na Massawe kwenye baa hiyo na kumfanyia mtoto huyo vipimo baa.
“Alex Massawe tulimkamata jana asubuhi akiwa wodi ya upasuaji baada ya kupokea kiasi cha Sh200,000 kutoka kwa Pamvelina Shirima ambaye alimleta mwanae afanyiwe upasuaji wa ngozi. Tunawataka wagonjwa wote kufuata taratibu ikiwamo kutokubali kurubuniwa na watu ambao hawajavaa sare wala vitambulisho rasmi ,” alisema Chisseo.
Kufuatia tukio hilo,Hospitali yaKCMC imethibitisha kuwa mtu huyo alikamatwa ndani ya hospitali hiyo, si mwajiriwa wao na wala hakukutwa na sare wala kitambulisho cha kitengo chake cha kazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema polisi itamfikisha mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika
 
Feki ni fashion kwa sasa Tanzania. Wakale wapi? Hata wagonjwa feki wapo. Ni kiasi cha kutaimiana tu.
 
Hata Rais yewezekana yupo feki...
 
Uongozi wa hospitali ya mkoani Kilimanjaro(KCMC) wamemkamata daktari feki,anayejulikana kwa jina la Alex Sumni Massawe. Anayejifanya ni daktari wa watoto,akiwa kwenye wodi ya upasuaji. Ameshikiliwa na jeshi la police. Source: magazeti ya leo
 
Mwisho tutasikia rais feki.
 
Hii sasa imezid... sa hapo kawekwa na nani jamani
 
Hawa ni ma co na AMO ambao hawataki kwenda shule. wako wengi sana na wizara ndio inawafuga.
 
Feki, feki, feki, feki, feki, feki...... Watanzania tumeridhika nazo ndo maana zinaongezeka kila leo.
 
Hata klabu ya Yanga juzi ilimgundua na kumtimua katibu mkuu feki!
 
Mkuu bora ya huyo maana ndo alikuwa anashughulikia maombi ya kazi akagundulika mapema kuliko feki zilizo kwenye system tayari.
 
UWE UNA-EDIT SIYO UNAKOPI TU ANGALIA HATA KURUKA MSTARI HUJUWI. By the way siku hizi kuna wagonjwa feki pia.

Tumekuwa tukisikia bidhaa feki, trafiki feki, ARV feki, madawa feki. Jamani watz nani atatuokoa na majanga haya? Ebu soma feki nyingine hii hapa chini:

KCMC yamnasa daktari feki akiandaa upasuaji
Na Rehema Matowo
Posted Alhamisi,Septemba5 2013 saa 20:27 PM
Kwa ufupi

Alikuwa wodi ya watoto akitaka kumfanyia upasuaji wa ngozi mmoja wa wagonjwabaada ya kuomba rushwa ya Sh200,000.

Moshi. Taharuki na hofu imewakumba wagonjwa waliolazwa katika Hospitali yaRufaa ya KCMC ya Mkoa wa Kilimanjaro, baada ya uongoziwa hospitali hiyo kumkamata daktari feki aliyekuwa na nia ya kumfanyia upasuaji wa ngozi, mmoja wa wagonjwa aliyekuwa hospitalini hapo na kutapeliwa Sh200,000

Alikamatwa katika wodi ya upasuaji akijinadi kwamba ni daktari wa watoto ametambuliwa kuwa ni Alex Sumni Massawe, ambaye alikamatwa jana asubuhi na makachero wa Polisi waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia baada ya uongozi wa hospitali hiyo kumuwekea mtego.

Kabla ya kukamatwa kwa Massawe, Mama mzazi wa kijana aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji wa ngozi, PamvelinaShirima alikutana na daktari huyo katika baa moja maarufu mjini hapa (jina limehifadhiwa) na kumtaka ampatie Sh200,000 ambazo atazitumia kuharakisha mwanae Makasi Tipesa afanyiwe vipimo.

Ofisa Uhusiano wa Hospitali hiyo,Gabriel Chisseo aliwaambia waandishi wa habari kwamba Massawe aliwekewa mtego na uongozi wa Hospitali ya KCMC kutokana na baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na daktari huyo feki. Alisema mama wa mgonjwa alipewa taarifa na rafiki yake kuwa anaweza kumpatia daktari atakayemsaidia kupata huduma kwa haraka,ambapo alimkutanisha na Massawe kwenye baa hiyo na kumfanyia mtoto huyo vipimo baa.

“Alex Massawe tulimkamata jana asubuhi akiwa wodi ya upasuaji baada ya kupokea kiasi cha Sh200,000 kutoka kwa Pamvelina Shirima ambaye alimleta mwanae afanyiwe upasuaji wa ngozi. Tunawataka wagonjwa wote kufuata taratibu ikiwamo kutokubali kurubuniwa na watu ambao hawajavaa sare wala vitambulisho rasmi ,” alisema Chisseo.

Kufuatia tukio hilo,Hospitali yaKCMC imethibitisha kuwa mtu huyo alikamatwa ndani ya hospitali hiyo, si mwajiriwa wao na wala hakukutwa na sare wala kitambulisho cha kitengo chake cha kazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema polisi itamfikisha mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…