kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Nchi hii iliyojaa vigogo wasioweza kufanya jambo bila maslahi yao binafsi kuwepo sasa inaenda kununua umeme toka Ethiopia. Ingefaa tuambiwe vizuri kama ni kwa faida ya nani maana jambo muhimu hapa kwa mwananchi wa kawaida ni kuona juhudi ambazo zimekua zikiendelea kwa kasi nzuri kusambaza umeme zinakamilika.
Licha hata kabla ya mashine zote za bwawa la nyerere kuwashwa tayari tumeambiwa umeme tumejitosheleza hadi tulipo. La ajabu unaona kila kigogo akipigana na mpango wake bila shaka kupiga dili. Kuna wanataka kuipa kampuni ya Adani ya india kusambaza umeme nchini wakati REA ishafanya kazi hiyo kwa weledi. Wengine ndio hawa wanataka tununue umeme toka Ethiopia. Wako vigogo wana mpango tuuze umeme nje hadi South afrika. Yaani kila kigogo au kundi la vigogo wanavuta ngozi kuwamba upande wao.
Kwa namna inaonekana vigogo hawana mpango wa wananchi ila mipango ya kushibisha matumbo yao.