Mchawi mwandamizi
Senior Member
- Jan 17, 2020
- 117
- 335
Habari zenu watanzania wenzangu, nawaomba msishtushwe na kichwa Cha habari nilichoweka hapo juu.mnaweza mkajiuliza "huyu anataka kusemaje tena?"😂 Au "muhuni au mwizi amefikaje kwenye jukwaa hili la stories of change"?
Twendeni kwa pamoja ili kujua NI kwa namna gani hili linaweza kuwa mkombozi wa taifa hili katika idara ya ujuzi katika kila kitu kilichopo duniani (everything in the world). Utekelezaji wake uwe kwa hatua au awamu Kama hivi au ifuatavyo;
Tuchague kwa makini tunacholenga 'kuiba' ujuzi wa kukitengeneza NI kitu gani hasa, na tukianza 'wizi wetu '(wenye manufaa makubwa kwa taifa) tusirudi nyuma Wala kujilaumu na kunyoosheana vidole, bila kusita, kwa mfano tuchague kutengeneza gari.
*Tanzania inapaswa kuwa na ujuzi wa kutengeneza magari katika ardhi ya Tanzania bila kutegemea wasimamizi toka nje, Kama hivi: tuchukue gari lolote lile (ambayo tayari tunayo nchini), tulifungue lote, tutenganishe kila sehemu, kila kipande, kila waya, kila kitu kiwe peke yake. Tuanze kufuatilia Kwanza kila kipande au kifaa kimetengenezwa kwa kutumia Nini au madini gani au malighafi gani, na yanapatikana vipi au wapi. Halafu Tuje kwenye kazi yake hicho kipande au kifaa ni nini, na bila hicho kifaa Nini kitatokea(siku hizi kupata taarifa SIYO ngumu kwa kuwa Kuna mitandao, utandawazi umekuwa sana).
*Tukishajua hayo tuje kwenye kutafuta malighafi za kuunda kila kipande kutokana na uchunguzi tulioufanya, Kisha tuunde kipande au kifaa Kama kile kile halisi Cha kwenye gAri husika tulilolifungua na kulitenganisha kila kitu kimoja kimoja. Tukiona tumeshindwa kutengeneza kifaa au kipande Cha kufanania basi tukae na kujadili kwa kurejea uchunguzi wa awali "kifaa au kipande husika kimeundwa na Nini hasa, malighafi gani ilitumika, iliandaliwa vipi, ilichanganywa vipi, katika mazingira gani?"
Tukishajua NI wapi tulikosea, basi turudie tena zoezi letu Hadi tufanikiwe kutengeneza kifaa husika kwa mfanano ule ule...Zoezi hili litakwenda kufanyika katika kila kifaa au kipande kinachounda gari iliyo nzima kimoja baada ya kingine. Tuhakikishe hatusahau kufanya utafiti kuhusu kila kifaa kina kazi gani na bila kifaa hicho Nini kitatokea, kwanini kinapaswa kiwe kifupi au kirefu au Cha rangi Fulani na SIYO rangi nyingine?
*Tukiweza hapo tunaingia katika Zoezi la kuanza kuvifunga (kuunganisha) vifaa tulivyovitengeneza wenyewe, kimoja baada ya kingine Hadi vyote viishe. Kisha tutalifanyia uchunguzi wa mwisho gari letu kabla ya kulijaribu. Kwa asilimia nyingi Kama sio zote gAri letu la Kwanza (gari lizawa😂) linaweza kuwaka na kuendesheka Kama tu lilivyokuwa gari tulilokorokochoa ili kuiba teknolojia.
SIYO GARI TU, hii iende kwenye kila kitu kilichopo duniani, kwa mtindo ule ule wa kufungua kila kifaa au kipande kisha kuchunguza kimeundwa kwa malighafi gani, zinachanganywa vipi, na kifaa kina kazi gani na bila hicho Nini kitatokea. Hili linawezekana kabisa tukiamua Kama nchi na kumaanisha adhma yetu. Taifa litapunguza utegemezi wa kuagiza Sana nje na Badala yake taifa litaweza kuuza nje. Kuiga ujuzi na kuuelewa sio mbaya hasa kwa taifa masikini kama Tanzania.
Jaribu kuwaza je NI kitu gani cha kibunifu au kiteknolojia taifa hili limeweza kutengeneza bila msaada wa watu wa mabara ya nje kwa mafanikio? jibu NI hakuna. Je, hii inamaanisha sisi hatuna utimamu Kama wenzetu wa mabara ya nje? elimu zetu tunazopata hazina uhalisia Kama elimu zao, Kama ndiyo kwanini tusiachane nazo na kuiga elimu za mabara mengine ambazo NI wazi Zina tija kwa mataifa yao na hata sisi tunaowategemea (kwa kuwa hata elimu tulizonazo kwa kiasi kikubwa ni kutokana na mifumo ya mabara mengine na SIYO afrika. sisi NI masikini sawa, je ni masikini wa kila kitu? Wenzetu wana kila kitu na sisi hatuna Kila kitu? SIYO kweli, tatizo ni moja TU kwamba huwa hatuwazi kumiliki ujuzi na hatujawahi kuwaza . Ili kuweza kupambania nafasi yetu Kama taifa la watanzania miongoni mwa mataifa yote duniani.
Woga na aibu kwamba tutaonekana vipi havisaidii kabisa linapokuja suala la kumiliki teknolojia (ujuzi), ukimiliki ujuzi unaheshimika popote pale duniani, na ndo maana watanzania wenye ahueni ya kimaisha hususani kiuchumi wakiumwa kwa asilimia kubwa hukimbilia kutibiwa nje hata ya bara kwa kuwa wanajua fika Tanzania haimiliki ujuzi Bali Ina watu waliofundishwa au kuelekezwa jinsi ya kutumia vifaa na kufanya baadhi ya Mambo kwa njia ya kusomea "fani" ukimiliki teknolojia iwe kwa kugundua mwenyewe au kwa kuiba ujue tayari umejikomboa pakubwa Sana serikali ina nyenzo zote za kuwezesha hili na Wala SIYO gumu kutekelezeka ni suala la kuamua na kuAnza tu, Na hii ndiyo Tanzania tuitakayo.
Asanteni.

Upvote
1