NCHI INAUZWA: Mwarabu Wa Oman Anayedai Kuwekeza Wa Airport Dar ALISHAINGIA MITINI Kuhusu ATCL

NCHI INAUZWA: Mwarabu Wa Oman Anayedai Kuwekeza Wa Airport Dar ALISHAINGIA MITINI Kuhusu ATCL

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,925
tanzania sold.jpg

Naomba niwe mkweli. Kila nikiskia Mwarabu flani anawekeza sehemu, hisia ya kwanza ni jinsi twiga na wanyama pori wetu wanavyotoroshwa na Waarabu...na sakata la Loliondo lililopelekea kifo cha mwandishi mahiri wa habari za Uchunguzi, Marehemu Stan Katabalo.


Kwa kifupi, picha iko hivi: Mwaka jana Rais Jakaya Kikwete alipokwenda huko Uarabuni, aliwahamasisha wafanyabiashara wa huko kuja kuwekleza Tanzania akidai kuwa nchi yetu ina "fursa zisizo na kikomo" (unlimited opportunities) kwa Waarab hao.

Kufuatia ziara hiyo ya JK na wito wake kwa Waarabu hao, siku chache baadaye (Januari mwaka huu) zikapatikana taarifa kuwa kundi la wafanyabiashara wa Oman likiongozwa na kampuni ya AL-HAYAT DEVELOPMENT AND INVESTMENT COMPANY wanapangakuwekeza dola za kimarekani milioni 100 kufufua shirka la ndege la Tanzania (ATCL), na memorundum of understanding ikasaniwa kati ya ATCL na bosi wa kampuni hiyo ya Oman Sheikh Salim Al-Harthy

Hata hivyo, mwezi Juni mwaka huu, Naibu wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba, aliliambia Bunge kuwa 'mwekezaji huyo wa Oman ameingia mitini' Kadhalika, Naibu Waziri huyo alieleza kuwa hakukuwa na makubaliano yoyote yaliyosainiwa kati ya 'wawekezaji' hao na ATCL

Cha kushangaza, vyombo mbalimbali vya habari huko nyumbani vimeripoti jana kuwa mtu yuleyule SHEIKH SALIM AL-HARTHY na kampuni ileile ya AL-HAYAT DEVELOPMENT DEVELOPMENT AND INVESTMENT COMPANY inatarajia kuufanyia ukarabati Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar, kwa kutumia uwekezaji wa dola za Kimarekani milioni 100.

Hivi ndugu msomaji, hata tukiweka kando rekodi ya 'wawekezaji' wa Kiarabu katika kuhujumu uchumi wetu, inaingia akilini kweli kwa mtu yuleyule aliyeleta uzushi kuhusu uwekezaji kwenye ATCL, na kisha kuingia mitini, kukabidhiwa dhamana ya kuifanyia ukarabari aiport yetu kuu?

'Mwekezaji' huyo Mwarabu alinukuliwa na gazeti moja akida (nanukuu)

"Nimekuja kuwekeza hapa kwa kuitikia mwito wa Rais Jakaya Kikwete, amechoka sana inabidi sisi tumsaidie, ana nia nzuri ya kuhakikisha nchi hii inakuwa kiuchumi inabidi tumsaidie kuwekeza katika maeneo kama haya" alisema. Katika hatua nyingine mwekezaji huyo ametangaza kuwekeza ndege nane kwenye Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL), mradi ambao unatarajiwa kugharimu dola za Marekani 100 milioni.

Tafadhali zinatia maneno hayo ya rangi nyekundu.

Cha kusikitisha zaidi, ni ukweli kwamba hata Waziri pekee anayeonekana kupigania haki za wanyonge, Dkt Harrison Mwakyembe, naye kaingia mkenge kwa kumsapoti Mwarabu huyo, na kunukuliwa akisema kuwa serikali imefanya kazi kubwa ya kuvutia wawekezaji hao...

NCHI INAUZWA: Mwarabu wa Oman anayedai kuwekeza wa Airport Dar ALISHAINGIA MITINI kuhusu ATCL ~ Kulikoni Ughaibuni

 
hulazimishwi kupanda hizo ndege za mwarabu, mabasi yapo mengi tu pamoja na fastjet.
 
hakika tanzania hakuna jambo zuri hata moja, nadhani huu ni ugonjwa mbaya
 
Hivi ni za Mwarabu au za ATCL?

Kulikuwa na uzi hapa kuwa ukifika Loliondo mitandao inapata signal za kuwa uko falme za kiarabu. Sijui kwenye hili la airport itakuwaje. Isije tukiwa tunajiandaa kutua kwa ndege wale air hostes watwambie SASA TUNATUA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA JNIA -uliopo oman
 
Kulikuwa na uzi hapa kuwa ukifika Loliondo mitandao inapata signal za kuwa uko falme za kiarabu. Sijui kwenye hili la airport itakuwaje. Isije tukiwa tunajiandaa kutua kwa ndege wale air hostes watwambie SASA TUNATUA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA JNIA -uliopo oman
":deadhorse:Etisalat"
 
Hii kitu tulishaijadili sana Mods unganisha hii kitu haina upya ni yale yale tu
 
nchi inauzwa watizedi kama mnapesa nunueni vipande tugawane. rais kachoka, si mnajua hadi muambiwe na wageni kuwa kachoka na sasa anasaidiwa kuiuza nchi uarabuni.sijui zamu hii kahaidiwa suti ama ni kanzu au ni ushauri wa namna ya kuongoza nchi na shekh asiye raia wa nchi ila mwenye uchungu na raisi wetu na pengine kiwanja chetu anajua yeye. tuombe nchi yetu isiwe ya kulipuana mabomu kama Baghdad na syria.amewashindwa wamwaga tindikali anaongeza wanaojilipua tena wanawaweka getini kabisa na vifaa vya kisasa.goshhhhhhhh
hivi huu mkataba hauna ka-ufisadi kwelii hapa.
 
Back
Top Bottom