Nchi inavyoliwa: OUT na mabonanza, kila mtu na kasungura kake!

siyabonga

Senior Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
125
Reaction score
35
Mambo yanavyoenda kwa hivi sasa tuko katika auto- pilot. Kila mtu anajaribu kuvuna karibu anavyoweza katika eneo lake. Madini, Mali Asili, Viwanda, Afya basi alimradi kila mtu anakula anavyoweza. Ukikipata kitumie, na ukikosa kijutie!

Hawa jamaa wa Chuo Kikuu Huria ni sherehe tu, party na mabonanza kila siku, sijui kazi wanafanya saa ngapi.

Wakitoka huko ni kujishughulisha na mambo ya Mamiss, mivinyo, safari na ubadhirifu. Wana kesi nyingi za wizi na ubadhirifu mahakamani.

Upo msururu wa watu ambao kwa miaka mingi hawajahitimu kwa kuwa papers zao bado hazijawa marked katika ngazi mbalimbali, idadi yao ya wanafunzi inazidi kushuka mwaka hadi mwaka. Hawana muda wa kufanya majukumu yao ya msingi.

Kwa mtaji huu, sijui kama tutafika. Udhaifu kila mahali, hakuna mwenye muda wa kumsimamia mwingine. KWELI HILI NI SHAMBA LA BIBI!
 
Wewe ni mmoja wa waathirika wa mambo ulioelezea hapa au umetumwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…