Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Baada ya vita ya Korea, Korea kaskazini ikaanza kuhangaika kujenga uchumi wake. Ikagundua kuwa ili iwe na uchumi imara inahitaji viwanda. Ikagundua pia, kuwa viwanda haviwezekani bila kuwa na chuma.
Ikasema ngoja iende Japan ikanunue kinu cha kufulia chuma. Marekani aliposikia habari hiyo akamuambia mjapan, usimuuzie huyo bwana chuma. Japan akasitisha kumuuzia.
Kiongozi wa North Korea akawaita wanasayansi akawaambia nataka tubuni na kutengeneza kinu chetu wenyewe. Baada ya muda wakawa na kinu chao na wakawa wanazalisha chuma.
China wakati wa Mao nao waligundua kuwa, bila chuma hawawezi kuwa nchi ya viwanda. Wakasema, kila balozi inatakiwa kuzalisha chuma. Tunahitaji ton kadhaa za chuma kwa mwaka. Basi watu wakajenga vinu vidogovidogo kila sehemu.
Kila familia ilitakiwa kushiriki kuzalisha chuma. Watu wakayeyusha vijiko na masufuria ili kufikia lengo. Chuma kilichopatikana hakikufaa lakini inaonyesha jinsi walivyopambana kupata chuma.
Leo hii China inaongoza kwa kuzalisha steel na kununua iron ore. Walitaka wajenge reli toka huko Liganga hadi Mtwara kwaajili ya kupeleka chuma kwao.
Kwa kweli nimeona kuwa hakuna nchi inaweza kuwa ya viwanda bila kuzalisha chuma. South Africa imeendelea kiviwanda , inazalisha chuma kwa kwa wingi sana.
Huwa watu wanasema "hata sindano tunaagiza?" Lakini huwezi kutengeneza sindano kama huna chuma. Kwa maoni yangu hii sera yetu ya viwanda ilitakiwa ianze na kuzalisha chuma. Tuna chuma huko Liganga Ludewa, Chunya na milima ya Uluguru.
Wakuu nyie mnaonaje, nchi inaweza kuwa ya viwanda bila kuzalisha chuma?