Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
NCHI INAZIDI KUFUNGULIWA, UKIZUBAA SHAURI YAKO.
Anaandika, Robert Heriel
Naona nchi inazidi kufunguliwa, wageni Kutoka Nchi za ng'ambo wanazidi kumiminika. Majiji makubwa yamesongwa na wageni wa tabaka za Kati na zajuu. Kazi kwenu vijana na wamama kuchangamka.
Nchi ikifunguliwa inakuwa na mambo mengi Kwa maana penye wengi kuna mengi. Nchi ikifunguliwa na watu wanafunguka, unajua nini kinatokea Watu wakifunguka? "Pesa, Pesa, Pesa × 3" hicho ndio kiitikio cha jibu la swali Hilo.
Majizi, Wezi, matapeli, wahujumu uchumi, dili zote hatari zinafunguliwa. Lakini pia zipo dili Safi na biashara halali zinafanyika. Hilo lisikutishe hiyo ni kawaida Kama nchi ikifunguliwa kwani inatoa fursa kila MTU kufunguka, kila mmoja ale Kwa urefu wa Kamba yake.
Lakini usije ukajichanganya ukafanya Dili chafu, dili haramu ukidhani nchi ikifunguliwa basi Sheria hazifanyi kazi, oooh! Sheria zipo palepale Ndugu watazamaji na wasomaji pàle😀😀.
Ukiamua kubaki kulalama, bakia hapohapo Wakati wenzako wapo speed 120 highway kwenye mteremko mkali.
Naomba Kwa heshima na taadhima nisiwaache bila kuwapa mbinu za kudili na nchi inapofunguliwa; ni kama ifuatavyo:
1. Hakikisha muda wote unabando, usipitwe na taarifa zozote za kisiasa na kiuchumi.
2. Anza Tabia ya kuangalia na kusikiliza Redio na linings channel za taifa kama TBC 1, Channel 10, Safari channel.
Mara mojamoja Angalia Cloud Tv hasa vipindi vya Maendeleo.
3. Anzisha biashara yoyote inayohusu kutoa Huduma au kuuza bidhaa.
4. Pendelea kutembelea maeneo yenye wageni wengi wa kigeni.
5. Wakati Watu wanalalamika vitu bei ghali, wewe tafuta namna ya kuvipata Kwa bei rahisi alafu uwauzie.
Nchi inapofunguliwa ni kawaida Maisha kuwa ghali na vitu kupanda bei lakini Pesa itakuwa inapatikana kirahisi.
6. Achana na mambo ya kupambana na wanasiasa au vyombo vya dola, wewe Kula nao sahani moja. Wasikusumbue nawe usiwasumbue. Msisumbuane.
7. Usikae kwenye line ya mwenzako, wala usikanyage waya.
8. Ukiingia kwenye dili haramu hakikisha unajua mlango wa kutokea, na Kwa vile wewe sio mzoefu, hakikisha usiwe incharge Kwa asilimia kubwa labda uwe muuza mchongo au ramani kuliko kuingia Field.
Zingatia Kwenye dili nyeusi wanapojaa Watu wengi itafikia Wakati WA kuwapunguza Watu ili biashara iwe stable. Watakaopunguzwa ni wale wadogowadogo wasio na uzoefu.
Hivyo inaweza kukugharimu.
9. Hakikisha unakuwa Katika silent mode au Low Key Wakati nchi ikiwa inafunguliwa. Wanasema Wakati WA Kula sio Wakati WA kupiga mayowe.
10. Ni Wakati na wewe wa kusafiri hata safari moja kuelekea hata hapo Dubai. Huwezi kosa milioni tano ya kukufikisha angalau nchi za nje. Huko ukikaa hata siku nne utakuwa umejifungua Kwa namna moja ama nyingine.
11. Nchi ikifunguliwa kesi haziwi nyingi kwa sababu kila mtu anafuraha, alafu mnaweza kumalizana wenyewe Kwa wenyewe pasipo kupelekana polisi au Mahakamani. Hivyo kama wewe ni MTU wa kupenda kesi kesi msimu huu unaweza kukusumbua.
Vijana ni Wwakati wa kuchangamka, kama haukuwahi kushika hata milioni 10 basi nchi ikifunguliwa ndio Wakati Sahihi Kabisa na uwezekano wa Kupata hizo Pesa.
Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Nipumzike SASA
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam