#COVID19 Nchi nyingine wananchi wanapinga chanjo ya covid-19 au ni Tanzania tu?

#COVID19 Nchi nyingine wananchi wanapinga chanjo ya covid-19 au ni Tanzania tu?

Michosho

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Posts
662
Reaction score
649
Nikiwa napitia mada mbali mbali hapa JF, kuhusu chanjo ya covid, nimekuwa nikisoma comments mbalimbali za wadau, juu ya hii chanjo ya covid19.

Wapo wanaopinga chanjo na wapo wanaotaka chanjo na tayari wengine wameshachanja. Ok fine,

Sasa Nimekuwa nikijiuliza, kwa kuwa suala hili la chanjo ni la dunia nzima. Je, Kuna nchi nyingine ambazo zoezi hili la chanjo halijapokelewa vyema na wanachi wake au ni Tanzania tu? Mfano wa nchi hizo ni zipi? Na je, Kuna nchi ambayo Hadi leo hii, hawajaagiza chanjo? wao sababu zao za kutoagiza chanjo ni zipi?

Na je, kama zipo na pengine ni nyingi, kwa Nini chanjo ikataliwe hivyo wakati madhara ya ugojwa wa covid,Delta na lambda wananchi wenyewe wanayaona?

(Yaani wananchi wanakufa Sana) kama tunavyoaminishwa na baadhi ya watu katika comments zao na media mbalimbali?
 
Back
Top Bottom