SoC02 Nchi ya Jamhuri

SoC02 Nchi ya Jamhuri

Stories of Change - 2022 Competition

Nasibu hemedi

Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
11
Reaction score
4
Nchi ya Jamhuri ilikuwa inaongozwa na katiba ya vyama vingi, katiba hio ilikuwa inaruhusu kila chama kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika nyanja mbalimbali za uongozi ili kurahisisha maendeleo ya nchi hiyo ya Jamhuri

Ila ifikapo mwaka 1980 kulikuwa na migogoro mingi sana kati ya jamii ya watu wa jamhuri na serikali yao
Chanzo cha migogoro ni kwa sababu mnamo mwaka 1719 nchi hiyo ya jamhuri ilipata uhuru wake kutoka kwa utawala wa Wasabilo ambao walikuwa wanalitawala taifa hilo la Jamhuri kwa takribani miaka 40.

Nchi hiyo iliruhusu mfumo wa vyama vingi lakini haijawahi kuwapa nafasi vyama pinzani kuongiza katika nafasi za juu mfano Raisi, wananchi walihoji kwanini kwanini chama pinzani wanabana sana wapinzani wao.
Wananchi walihoji kwa muda mrefu bila majibu mpaka hivi sasa bila kupata majibu sahihi hivyo ikawalazimu kunyamaza na maumivu moyoni.

Wananchi wa Jamhuri walikuwa hawajui umuhimu wa vyama vingi ila wao walikuwa wanalalamikatu juu ya siasa na viongozi wao bila kuzingatia mambo ya msingi yaliyokuwa yanaitajika nchini kwao.

Nchi hiyo ilikuwa haina shule za kata haina hospitali za kata wala haina mahakama za mwanzo lakini wao hawakuhiji juu ya haya.


MAMBO YANAYO HITAJIKA KATIKA NCHI YA JAMHURI

- Maji safi na salama kwa wanachi wishio mijini na vijijini kwa wakati​
- Elimu bora kwa kila mwananchi wa jamhuri​
- Huduma bora ya afya kwa kila mwanachi wa jamhuri​
- Miundombinu bora mfano barabara na umeme​
MAMBO YASIYO HITAJIKA KATIKA NCHI YA JAMHURI ILI KUONDOA MIGOGORO NI KAMA YAFUTAYO
- Kuepuka migogoroa kati ya wananchi na viongozi wanchi hiyo​
- Kila mwananchi ashighulike kwenye zoezi la kupiga kura ili wapate kiongizi wanao muhitaji kwa maendeleo yao.​
- Serekali ya jamhuri ikubali kukosolewa pale kunapojitokeza hitilafu kwenye uongozi​
- Serikali ijali wananchi wao zaidi kuliko kujali matumbo yao binafsi​
- Serikali iwaelimishe wananchi jinsi ya kujiajiri na kuwapa furusa bila vikwazo​


Je, serikali bora inatakiwa iwe na vitugani ili kuongoza kwa usawa na ufanisi?
(a) Viongozi wasiwe wa binafsi yani wasiwe wanatizama matumbo yao pekeyao na kuwakandamiza wananchi wao​
(b) Kiongozi anapokosolewa asichukulie kama amevunjiwa heshima bali achukulie ni sehemu ya kupata funzo na kuwa kiongozi bora kwa wananchi wake​
(c) Majeshi na vyombo vyote vya usalama wasimsifie kiongozi kwa unafiki kwa sababu hii italeta sintofahamu kati ya wananchi na pia humfanya kiongozi ajione bora kumbe hayupo bora kwenye uongozi wake ni sifa za kinafiki.​
(d) Wananchi wawe wanawasilisha malalamiko yao kwa utaratibu nzuri na umoja sio kila mtu anaongea lake.​
(e) Serikali iliyopo madarakani iepuke kuvibana vyaman pinzani kwa hua hii hupunguza ufanisi na ushirikano baina wa vyama hivyo na wananchi wao hupoteza imani ya utawala​


Umuhimu wa vyama vingi kwenye nchi ya jamhuri.

(a) Kutanua wigo wa siasa katika nchi husika​
(b) Huleta democrasia kwa nchi ya jamhuri​
(c) Kumpa uhuru mwananchi kuchagua palipo sahihi​


MADHAIFU YA KATIBA YA NCHI HIYO

(a) Katiba haikuweka kiwango au muda wa kila kiongozi kutawala na kusataafu kwa mujibu wa sheria​
(b) Katiba haikuweka kumlazimisha kiongozi wa chama pinzani kupewa uongozi kwa mujibu wa sheria​
(c) Katiba huwa inampa uhuru kiongozi aliopo madarakani kumchagua na kumteuwa kiongizi ajae hii ni kasoro kubwa kwenye uongozi.​


Nini wanapaswa kufanya viongozi wa nchi ya Jamhuri?

(a) Kupunguza garama za maisha kwa wananchi wanaoteseka bila ajira na elimu ili kujenga jamii iliyo bora kwa maisha ya mbeleni​
(b) Kupunguza matumizi ya pesa za serikali yasiyo lazima ili kuoata fedha za kutosha za kujengea miundombunu ya jamii angalau kwa 50%​
(c) Kupunguza kwa safari zisizo za lazima kwa baazi ya viongozi ili serekali iweze kubaki na pesa kwa ajili ya kupunguza ugumu wa maisha kwa wananchi wake​
(d) Kuweka sheria kali na thabiti ya kuwakamata wote wanao ihujumu serekali ya jamhuri kwa kipingi hichi kigumu inayo pitia.​
(e) Kubadili mfumo wa bunge badala ya wabunge kupeleka hoja bungeni pekeyao kuwe na wawakilishi wengine wanao peleka malalamiko ya wanachi moja kwamoja kwa Jili ya utatuzi wa zarura sio mpaka bunge likae kwanza​
(f) Viongozi wa nchi ya jamhuri wote wajuu mfano maziri na na raisi wawe na utamaduni wa kutembelea wananchi kwa kipindi kifupi yani kila mara hii huwafanya wananchi wao kuwa na imani na viongozi wao.​
(g) Serikali ya jamhuri huoaswa kubadili katiba mara kwa mara ili kuendana na maitaji ya jamii kwa wakati ule kwakuwa katiba ibapo kaa kwa muda mrefu hupoteza uhalisia na ubora wake na kuto jitosheleza kwa jamii husika.​

Lakini wananchi wa nchi ya jamhuri kama watafanikiwa kuungana pamoja na viongozi wao katika kuketa maendeeleo watapata mafanikio yaliyo bora kwq kuwa umoja ni nguvi utengano ni uzaifu.

Hivyo kupitia historia ya mchi ya jamhuri tunapaswa kubadilika na kujifunza ili kupata huduma zilizo bora bila kuwalaumu viongozi wetu.

Hususani katika nchi zetu za Afrika kwakua ndizo nchi zinazo kubwa na aina ya majanga kama yanavyo ikumba nchi ya jamhuri tangu kupata uhuru mpaka hivi sasa.

Tusisahau kumuomba mungu na kumtanguliza kwa kila jambo kwakuwa hakuna binadamu asio na imani.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom