SoC03 Nchi ya kusadikika ambayo kila mwalimu wa kitanzania anaitamani

Stories of Change - 2023 Competition

cupvich

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
408
Reaction score
247
"Baba Wande amka unachelewa kazini" ilisikika sauti ya Mke wa mwalimu Matinyi ambaye ni mwalimu wa somo la hisabati katika shule ya sekondari MAPWE. Kwa haraka mwalimu Matinyi aliangalia saa yake na kugundua kuwa ni saa kumi na moja na dakika kumi alfajiri,alikumbuka kuwa yuko zamu kwa wiki hiyo, hivyo alianza maandalizi haraka kwa ajili ya kuelekea kazini. Wakati anaendelea na maandalizi mwalimu Matinyi ambaye ana miaka kumi kazini alionekana mwenye huzuni jambo ambalo lilimstua mke wake. "Baba Wande mbona leo hauna furaha" mama wande aliuliza, " NATAMANI NINGEKUWA NAFANYA KAZI KATIKA NCHI YA KUSADIKIKA" mwalimu matinyi alimwambia mke wake huku akipanda baiskeli yake na kuelekea kazini wakati mvua ikiendelea kunyesha taratibu.

" Niko zamu, mimi ndiye mwalimu pekee wa hisabati shuleni kwangu, zaidi ya wanafunzi 1000 wananitegemea hivyo siwezi kuacha kwenda kazini" Alijisemesha mwalimu Matinyi huku akiendesha baiskeli yake katika barabara ya tope kuelekea shuleni MAPWE iliyo umbali wa kilomita 20 kutoka anapokaa huku ikiwa umbali wa kilomita 120 kutoka yalipo makao makuu ya Halmashauri. Shule ya sekondari Mapwe haina nyumba hata moja ya mwalimu na hata katika kijiji cha MAPWE kilichopo katika Kata ya MAPWE hakuna nyumba za kupanga hivyo walimu hulazimika kuishi katika kata ya jirani iliyopo umbali wa Kilomita 20.

Alifika shuleni saa mbili na robo akiwa amechafuka kutokana na matope, nguo zake zikiwa zimelowana huku akiwa ndiye mwalimu wa kwanza kufika. Bila kujali hali yake aliamuru kengele igongwe, wanafunzi wote wakakusanyika. " POLENI NA CHANGAMOTO YA MVUA WANANGU, SASA NI MUDA WA KUINGIA DARASANI NAOMBA KILA MMOJA AELEKEE KATIKA DARASA LAKE NA KUENDELEA KUJISOMEA WAKATI TUKIWASUBIRI WALIMU WENGINE" mwalimu Matinyi aliwatangazia wanafunzi wake. Shule ya sekondari Mapwe ina jumla ya wanafunzi 1204 huku ikiwa na walimu saba wote wa kiume, walimu wa kike hulazimika kuhama baada ya kuajiriwa kutokana na changamoto ya makazi na Miundo mbinu isiyo rafiki kumuwezesha mwalimu kuishi karibu na shule.

Akiwa ametulia ofisini, mwalimu Matinyi alitafakari mazingira magumu anayofanyia kazi yeye pamoja na walimu wenzake, Alikumbuka kuwa siku iliyopita alifunga safari yapata kilomita 120 kwenda makao ya halmashauri anayofanyia kazi mwendo wa saa tano kwa gari ili kushughulikia Madai yake ya LIKIZO na MAPUNJO ya mshahara lakini hakufanikiwa zaidi ya kujibiwa majibu ya kukatisha tamaa na wahusika jambo ambalo lilimuumiza sana kiasi cha kulala usingizi mzito Usiku huo na kuota Ndoto ya NCHI YA KUSADIKIKA AMBAYO KILA MWALIMU ANAITAMANI.

"Mwalimu matinyi mbona Unaongea peke yako uko sawa kweli?"
ghafla aliiingia mwalimu mwenzake na kumkuta akiongea peke yake. " Hapana mwalimu niko sawa" alijibu mwalimu Matinyi huku akichukua Chaki na kuelekea darasani. Alingia darasa la kidato cha kwanza kufundisha, akiwa katika kufundisha huku akiwa mtu mwenye mawazo sana, alimuona mwanafunzi mmoja wa kike aliyekuwa anaitwa Ajina akiwa anaongea. "WEWE NJOO HAPA" alimuita Ajina kwa hasira. Alichukua fimbo na kuanza kumuadhibu Ajina. Ghafla Ajina alipoteza fahamu na kudondoka chini huku akitokwa na damu puani na masikioni?. MASIKINI MWALIMU MATINYI!!!!! Kutokana na kelele za wanafunzi, walimu waliokuwa madarasa mengine waliwahi katika lile darasa na kumkuta mwanafunzi Akija akiwa amepoteza fahamu huku akitokwa na damu nyingi wakati mwalimu Matinyi asijue la kufanya.

Uongozi wa shule ulimkimbiza Akija kituo cha afya kwa ajili ya matibatu na wazazi wake wakataarifiwa. Mwalimu Matinyi akiwa amejaa woga alichukua baiskeli yake na kuanza kurudi nyumbani.Alifika nyumbani na kumkuta mke wake akiwa kibarazani akimsubiri kwa hamu kwasababu asubuhi hakuondoka vizuri. " Mbona umewahi kutoka kazini na sio kawaida yako mme wangu?" Aliuliza Mama wande. Mwalimu matinyi hakumjibu chochote bali alimuomba amletee maji ya kunywa. Mke wa mwalimu Matinyi alikumbuka kauli ambayo aliitoa mme wake asubuhi wakati anaenda kazini kwamba NATAMANI KUFANYA KAZI KATIKA NCHI YA KUSADIKIKA, "mme wangu ulimaanisha nini uliposema hivyo?" Aliuliza mke wa mwalimu Matinyi, huku akihisi kuwa mme wake hayuko sawa.

Mke wangu! Jana niliota Ndoto ambayo niliifurahia sana na nilihuzunika sana uliponiamsha kwani sikuendelea kuota tena. " Ndoto ipi Mme wangu" aliuliza mama Wande. "Niliota ninaishi na kufanya kazi katika nchi ambayo MWALIMU anathaminiwa na kupendwa na kila mtu, Nchi ambayo serikali yake imempa kipaumbele mwalimu kutokana na umuhimu wake katika jamii, Nchi ambayo mwalimu analipwa mshahara mzuri, Nchi ambayo hakuna mwalimu anayeidai serikali MAPUNJO WALA PESA YA LIKIZO, nchi ambayo mwalimu anapanda madaraja kwa wakati, Nchi ambayo kila shule ina nyumba za walimu na kwa shule ambazo Nyumba za walimu hazitoshi Serikali inatoa fedha kwa ajili ya pango la mwalimu, Nchi ambayo mwalimu analipwa posho ya kufundishia na posho ya mazingira magumu, Nchi ambayo walimu wanatosheleza katika kila shule.

Mwalimu Matinyi aliendelea kumsimulia mke wake ndoto aliyoiota usiku huku mke wake akimsikiliza kwa makini, Katika nchi ile mwalimu anafuatwa katika kituo cha kazi ili kupewa huduma na mamlaka zinazohusika ili asipoteze vipindi vyake, Mazingira ya ofisi za walimu zikiwemo meza na viti wanavyokalia walimu pamoja na chakula wanachokula wakati wakiwa kazini ni jambo jingine ambalo nililifurahia sana katika nchi ile. Hakika walimu katika nchi ile wanafanya kazi kwa raha na kuifurahia kazi yao, hata maisha yao ni mazuri sana kiasi cha kila mtu kutamani kuwa mwalimu. HII NDIO NCHI YA KUSADIKIKA AMBAYO KILA MWALIMU ANAITAMANI" Alimaliza kusimulia na kumfanya mke wake kushikwa na butwaa. Ghafla Ujumbe mfupi unaingia katika simu ya mwalimu Matinyi aliyokuwa ameishika " Mwanafunzi wetu AJINA ameaga dunia". Mwalimu Matinyi asijue la kufanya kwani Mwanafunzi Ajina ndiye yule aliyemchapa darasani akazimia.

Uoga ulimuingia na kuona Maisha yake yapo hatarini kwasababu adhabu yake imesababisha kifo cha mwanafunzi. " NENDA UKANINUNULIE VOCHA NIFANYE MAWASILIANO" mwalimu Matinyi alimwambia mke wake huku akimpatia pesa. Asijue nini kinaendelea mke wa mwalimu Matinyi alianza safari kuelekea katika duka lililo umbali wa kama nusu saa hivi. Baada ya kuhakikisha kuwa mke wake amefika mbali, mwalimu Matinyi aliingia chumbani, akachukua karatasi na kuandika "APUMZIKE KWA AMANI MWANAFUNZI WANGU AJINA, NINGEKUWA NAFANYA KAZI KATIKA NCHI YA KUSADIKIKA HAYA YOTE YASINGETOKEA, SERIKALI HAINA BUDI KUWAPELEKA WALIMU WOTE WA TANZANIA KATIKA NCHI YA KUSADIKIKA". Baada ya kumaliza kuandika maneno hayo aliiweka katatasi hiyo sehemu ya wazi kisha Akachukua kamba na KUJINYONGA.
 
Upvote 7
Safi mdau

Je unashauri nini mwalimu ambae ndio anaingia kwenye ajira mpya nini afanye nini ili aweze kujikimu kimaisha /ukilinganisha mwalimu kwa sasa anabanwa na shule baada ya mda wa kazi Kuna masomo ya ziada, jumamosi Bado anahitajika kusimamia mtihani ya week sasa apa nini mwalimu afanye aweze kutoka kimaisha
 
Mimi ni mwajiriwa mpya mnashauri nifanye nini ili niweze kufanya biashara zangu bila kuathiri Kazi yangu ya kufundisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…