Nchi ya Rwanda na Rais wake Paul Kagame wamekuwa mfano bora na wa kuigwa katika kupambana na COVID-19

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Serikali ya Rwanda kupitia Rais wake imefanya yafuatayo..

1. Inawajali Wananchi wake mara kwa mara juu ya Ugonjwa
2. Inatoa Msaada wa Vyakula bure kabisa kwa Wananchi wake
3. Inatoa bure kabisa Vifaa vya Kujiinga na Ugonjwa kwa Wananchi wake
4. Waziri wake wa Afya hana Unafiki katika Kutoa Taarifa sahihi kwa Wananchi
5. Kwa Rwanda huu Ugonjwa siyo wa Aibu au wa Kuficha kwa Jumuiya ya Kimataifa
6. Viwanja vya Ndege na Mipaka yote Umakini umeongezeka na Kudhibitiwa
7. Imeunganisha nguvu na Jumuiya ya Kimataifa katika Kutafuta Suluhu ya Ugonjwa duniani

Serikali zingine duniani na Marais wao wamefanya yafuatayo

1. Wanaficha Taarifa za Wagonjwa kwa Wananchi wao
2. Marais wao wanajificha Kuuongelea wakidhani ni Ugonjwa la laana
3. Mawaziri wao wa Afya wakizungumza ni Kuchekacheka tu kama Ngiri na Mizaha mingi
4. Wananchi wao wanajazana hovyo hadi Kujambiana sana katika DalaDala
5. Wanajali sana Mapato ya Kodi kuliko kujua idadi ya Wagonjwa wanaoongezeka
6. Wanaficha Taarifa za Ugonjwa ila chini chini wanaomba Misaada ya Pesa WB
7. Viongozi wao wanakataza Mikusanyiko ila wao wakiongea wanakusanya Watu wengi

Nchi zingine za Afrika bado hajizachelewa Kuiiga Rwanda na hasa Kumuiga Rais wake Mahiri na bora kabisa Paul Kagame.
 
Mbona sioni jipya hapo nchi zote kasoro sisi na Burundi zimefanya hivo............acha 'egoism' mkuu
 
Hapa kwetu nchi imejaa wapuuzi watupu.

Wanarundika watu kwenye vituo vya mwendokasi kusubiri level seat wakati mrundikano vituoni unakuwa mkubwa zaidi na watu wanachukua muda mrefu zaidi kuliko kubanana kwenye gari kwa dakika tano tu.

Wamechukua measures sawa lakini kwanini ziwe za kingumbaru namna hii ?
 
Sent using Jamii Forums mobile app

Kichwa kikiwa ni ' Debe Tupu ' au ' Kichwa Maji ' kamwe huwezi kuona Jambo jipya hasa kwa wale ambao kidogo Mwenyezi Mungu aliwabariki Upeo mkubwa na Maarifa mengi kuliko Wewe.
 
Kumbe ni wewe Popoma.Kagame atashindwaje kuhudumia hako ka Kijiji,hata wewe ukiwa Raisi wa Rwanda utaweza kuwalisha na kuwataza Wanyarwanda wote,lakini siyo li nchi la Tanzania.Hili ni bara Mzee

Sent using Jamii Forums mobile app

Katika Maelezo yangu nimeitaja mahala popote nchi yako ya Tanzania? Acha ' Kuwashawashwa ' tafadhali na Siku zingine jikite katika Kuuelewa Uzi kuliko Kukurupuka katika Kuukabili mwishoni ukaja kuonekana ni Popoma wa Kutukuka.
 
Rwanda ina watu kama wa ubungo pekee ndio unalinganisha na watu mil 63

Tumia akili kufikiri

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama Rwanda haina ' Rasilimali ' nyingi kama zilizoko nchini Kwako lakini Rais wake anaweza Kujibana na Kuzitumia hizo hizo ndogo na nchi yake inaenda na hata Kuiacha yako Kimaendeleo je, huoni kuwa Wewe ambaye una ' Rasilimali ' nyingi ( lukuki ) na idadi hiyo Kubwa ya Watu lakini hamna mbele wala nyuma mtakuwa na ' Upopoma ' mwingi? Nasubiri jibu lako juu ya hili tafadhali.
 
Hapa kwetu nchi imejaa wapuuzi watupu.

Wanarundika watu kwenye vituo vya mwendokasi kusubiri level seat wakati mrundikano vituoni unakuwa mkubwa zaidi na watu wanachukua muda mrefu zaidi kuliko kubanana kwenye gari kwa dakika tano tu.

Wamechukua measures sawa lakini kwanini ziwe za kingumbaru namna hii ?

Sent using Jamii Forums mobile app

Samahani Mkuu hapa unaiongelea nchi gani labda?
 
Serikali ya Rwanda kupitia Rais wake imefanya yafuatayo..

1. Inawajali Wananchi wake mara kwa mara juu ya Ugonjwa
2. Inatoa Msaada wa Vyakula bure kabisa kwa Wananchi wake
3. Inatoa bure kabisa Vifaa vya Kujiinga na Ugonjwa kwa Wananchi wake
4. Waziri wake wa Afya hana Unafiki katika Kutoa Taarifa sahihi kwa Wananchi
5. Kwa Rwanda huu Ugonjwa siyo wa Aibu au wa Kuficha kwa Jumuiya ya Kimataifa
6. Viwanja vya Ndege na Mipaka yote Umakini umeongezeka na Kudhibitiwa
7. Imeunganisha nguvu na Jumuiya ya Kimataifa katika Kutafuta Suluhu ya Ugonjwa duniani

Serikali zingine duniani na Marais wao wamefanya yafuatayo

1. Wanaficha Taarifa za Wagonjwa kwa Wananchi wao
2. Marais wao wanajificha Kuuongelea wakidhani ni Ugonjwa la laana
3. Mawaziri wao wa Afya wakizungumza ni Kuchekacheka tu kama Ngiri na Mizaha mingi
4. Wananchi wao wanajazana hovyo hadi Kujambiana sana katika DalaDala
5. Wanajali sana Mapato ya Kodi kuliko kujua idadi ya Wagonjwa wanaoongezeka
6. Wanaficha Taarifa za Ugonjwa ila chini chini wanaomba Misaada ya Pesa WB
7. Viongozi wao wanakataza Mikusanyiko ila wao wakiongea wanakusanya Watu wengi

Nchi zingine za Afrika bado hajizachelewa Kuiiga Rwanda na hasa Kumuiga Rais wake Mahiri na bora kabisa Paul Kagame.

Umelazimishwa uishi Tanzania mkuu?nenda kaishi Rwanda

Sent using IPhone X
 
Kuna nchi magavana uchwara wanakusanya watu na kuanza kuhubiri "upumbavu"...Eti wenye nyumba washushe kodi kwa 50%,Kwani kuna lockdown?..Mishe si zinaendelea?
 
Kwani huu Uzi unazisema nchi zingine duniani au Tanzania yako tu pekee? Kuna Watu mna matatizo makubwa sana ya Akili Ulimwenguni.
 
Kuna nchi magavana uchwara wanakusanya watu na kuanza kuhubiri "upumbavu"...Eti wenye nyumba washushe kodi kwa 50%,Kwani kuna lockdown?..Mishe si zinaendelea?

Mkuu Mimi nipo hapa Malawi je,ni nchi gani hiyo wenye Nyumba wameomba Kupunguza Kodi?
 
Back
Top Bottom