Nchi ya wajinga

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Posts
392
Reaction score
949
Tanzania si ya Nyerere,
Ujamaa hadi ruhusa,
SabaSaba ni NaneNane,
Mkulima hana sauti,
Mfanyabiashara ana sauti,
Viongozi hamna leo,
Mwanasiasa ndio viongozi.

Tanzania si ya Nyerere,
Zuia gazeti kuna whatsapp,
Funga Tv kuna facebook,
Zuia radio kuna blogspot.

Tanzania si ya Nyerere,
Wabunge wananuliwa,
Teknolojia hainunuliwi,
Teknolojia ni ya Nyerere,
Elimu hainunuliwi,
Elimu yetu lugha mbili,
Elimu yetu ni duni,
Elimu ya mtahara duni,
Tanzania si ya Nyerere.

Bunge halina nguvu,
Bunge haliamui,
Bunge lina-amriwa,
Bunge halichagui,
Bunge linachaguliwa.

Tanzania si ya Nyerere,
Uongozi umekuwa ajira,
Fisadi yupo uraini,
Mwizi kuku yu gerezani,
Watanzania wengi wajinga,
Wachache wanaojielewa waoga,
Wachache wanaojielewa hupotea ghafla.

Tanzania si ya Nyerere,
Kuwa CCM usikilizwe,
Kuwa CCM usautiwe,
Kuwa CCM ushibe,
Kuwa CHADEMA ununuliwe,
Vyama pinzani wajinga,
Ujinga wao wa dola,
Wapate dola walete maendeleo,
Maendeleo huletwa na Dola tu?
 
nchi ya wacheza biko na tatu mzuka, hatari saana kaka.
 


Nilipoweka rangi,Upinzani Tanznaia ni uadui,ingekuwa nchi za wenzetu tungeona tofati kubwa sana.Ukiwa mpinzani unatakiwa ukosoe,lakini kwa kwetu ukiwa mpinzani hata pesa za maendeleo jimboni hazipelekwi hayo maendeleo unapeleka na nini?


Pili ungeweka na para ya Mahakama maana nazo hazina hadhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…