Tanzania ni Nchi yenye neema nyingi na Kila namna. Neema zetu kiroho, kimwili, kijamii na kiuchumi zinaifanya Tanzania kuwa kama mtoto aliyezaliwa akiwa na hamu ya Nini kinafuata.
Kunyonya kwa mama kunaamsha matamanio ya kesho yenye kicheko. Watanzania ni watu wenye matumaini ya kesho nzuri.
Mwaka 1964, safari yenye ndoto na matamanio mazuri ilianza chini ya kiongozi aliyejinasibu Kwa kuacha yote ya binafsi Kwa kufuata faida ya wengi.
Kuacha kazi ya ajira au kupambana na mkoloni Kwa nguvu ya hoja halikuwa jambo rahisi. Julius Kambarage Nyerere aliiongoza Tanzania kuwa na katiba yenye kutaka Uhuru na umoja ili kutimiza ndoto za Kuwa huru. Msisitizo wa yaliyomo uliegemea katika harakati nyingi.
Kila mara ninaota vijiji vya ujamaa na kujitegemea ambamo Kila mkazi ni mchapa Kazi anayerudi jioni na kufurahia familia yenye amani na furaha yenye nidhamu na chakula Cha kutosha.
Natamani kuamka SIKU Moja nikute njia zote za miji zimejaa raia walioandika mioyo yao "ujamaa na kujitegemea" jambo ambalo lazima liwekewe misingi maalum hasa hasa!!!
Nawaona viongozi wa kiroho wakitoa mchango mkubwa kuwaandaa Watanzania huko makanisani. Hawa, wanawafundisha waumini kufanya kazi, kupendana, kuwa mazao yenye kutosha kusaidia yatima na wajane, msisitizo wao wa kiwepo Amani na kuvumiliana inawapa hata viongozi wa kisiasa urahisi wa utendaji.
Natamani kuona serikali zikiwatambua na kiwapa kipaumbele chenye lengo la kurahisisha kazi Kwa kuwa katika Kila mlango watatoka raia ambao Wana amani na uvumilivu unaotokana na kushiba neno la mtume au wakristo ambao biblia imewabadili maisha na kuwaweka mahali pa raha yao.
Katika Hali hiyo kuongoza kunakuwa rahisi kama kusukuma baiskeli isiyo na upepo kwenye tairi zake katika mteremko wenye utelezi. Ni Tanzania ambayo viongozi wa kiroho wanarahisisha kazi za wakusanya Kodi, watafsiro Sheria na Kila nyanja.
Nawaona Watanzania wa kesho ambao kimwili wamejaa afya tele na furaha inayowawezesha kuamka na kuifanyia siku yanayoipasa Hadi inafaa kuitwa siku.
Kila raia anakuwa na bustani yenye mboga, matunda na mifugo michache Kwa chakula hasa Cha familia. Kila mwanafamilia anafurahia protini na wanga na vitamin iliyotoka katika mazingira ya nyumbani bila sumu Wala nyongeza za wataka faida.
Afya ya mwili Kwa Kila familia inawafanya kushiriki katika maisha ya Kila siku katika namna ya kuleta vingi vilivyo chanya nyumbani.
Baba, mama, watoto na ndugu wenye afya wanafanya jamii yenye uzalishaji mkubwa. Naota Watanzania wenye afya inayowafanya kuzalisha zaidi, furaha zaidi na amani zaidi.
Tanzania ambayo Kila raia yuko safi kimwili, mwenye afya inayompa hamu ya kuchapa kazi ili kukidhi mahitaji binafsi na familia Kwa kutosha.
Inawezekana kuwa na Nchi ambayo watu wake kimwili wanasongesha maisha Kila Kona. Kila mmoja ana moyo wenye kuridhika kutenda majukumu bila kusukumwa.
Kijamii tutaamka asubuhi ya kesho yetu tukiwa na watu wenye ushiriki mkubwa wa kutawalika na kufurahia matunda ya uongozi Bora Kwa kuwa Kila mmoja anatoka katika familia yenye mema mengi. Jamii iliyoandaliwa vizuri kutoka huko kanisani na misikitini inawaleta raia wazuri, inawaleta viongozi wenye hofu ya Muumbaji na watoto waliolelewa wakaleleka.
Mambo hasi kama talaka, ugomvi na uhalifu haviwezi kupata nafasi katika Tanzania ya kesho. Milango ya mambo hasi itafungwa na funguo kutupwa katika kina kirefu Cha bahari. Jamii Bora itazaa raia Bora na viongozi Bora wenye hofu ya rushwa naambo yote mabaya.
Kesho itapata wananchi walio na nafasi kubwa ya kwenda shambani na nafasi kidogo sana ya kwenda hospitali. Naiona siku tunaamka tunawakuta wananchi ambao tamaduni zao zinawafanya wale kile tu chenye afya, wafanye mambo tu mema. Inawezekana kabisa.
Serikali imewahi toa tamko, "tunataka Kila mkoa na wilaya kuwa na veta ambazo vijana wetu watapata ujuzi ili wakaanzishe viwanda na waweze kujitegemea", waziri mkuu Kasimu Majaliwa aliwahi sema. Tanzania ya kesho itakuwa na vijana wenye ufundi na stadi za Kila aina.
Kila kijana aliyemaliza shule anakuwa anao ufundi wa aina Fulani. Habari njema ya kuweka katika mitaala ya kielimu ufundi wa aina Fulani kuanzia Elimu msingi kunafanya suala la Kila mmoja kuwa na jambo la kufanya kuwezekana kabisa.
Hii itafanya kusiwe na mtu anayeitwa mzurulaji, ni kama Nchi ya kufikirika lakini hebu tulipe usingizi na kuamka katika Nuru ya pekee na uchumi wenye kuyafanya maisha yawe maisha.
Kila raia Kwa kuwa na kazi ya kufanya atakuwa na kipato Wala hatalazimishwa kulipa Kodi zaidi ya kuipeleka mwenyewe Tena Kwa raha na roho nyeupe. Uchumi wa Nchi kesho utakuwa umeimarika Kwa uzuri wenye kukua Kila iitwapo leo.
Njozi hizi za serikali kuhusiana na kuboresha mitaala Zina kesho nzuri sana sana.
Utamaduni ni jumla ya maisha ya Kila siku ya watu. Hii inahusu chakula, lugha, mavazi na mambo yote ya kiimani. Watu wanaosali na kushiriki shughuli za Kila siku kama ilivyoelezwa hapo juu, ni muhimu kwamba watazalisha jamii Bora.
Kesho tutakuwa na Tanzania ambayo watu wake wanakula vile vyenye afya, wanavaa mavazi ya heshima na staha, wanaongea lugha yenye adabu na staha wanashiriki katika mambo ya kiimani yenye tija na yanayoleta mantiki katika maisha ya Kila siku. Kazi inakuwa sehemu ya utamaduni wa watu.
Asiyefanya kazi anaongozwa kuwa na kitu Cha kufanya Kwa kupata stadi za maisha. Tanzania inakuwa Nchi yenye utamaduni Bora katika dunia.
Katika Hali hii hata wanaoeneza ushoga au ulawiti hawawezi kupata nafasi ya kujipenyeza katika Tanzania ya kesho. Hii ni kesho ambayo huwezi kusikia ugomvi Wala wizi.
Kila familia inasimamia utamaduni Kwa kuweka misingi ya kuvaa kula na kutenda kile tu kinachokubalika na jamii Tena kilicho chema tu. Itakuwa Nchi ambayo watu wake Wana asilimia kubwa sana ya watu wenye amani.
Hatimaye ndoto ya Tanzania yenye matumaini inakuwa halisi. Kama Muasisi wa taifa letu akiamka anaweza kusema Asanteni Kwa Tanzania hii, ndiyo hasa niliyoitaka.
Natamani kuiona Tanzania ya namna hii. Ni ndoto ya dhahabu iliyozungukwa na almasi juu ya Tanzanaiti iliyo pekee Tanzania tu.
Kisha najiuliza iwapo polisi, mgambo, wakusanya Kodi na askari jela kama watakuwa na kazi kubwa ya kufanya Zaidi mikutano ya kusifia kuwa na jamii nzuri namna hii na kutoruhusu wabaya kuingia na kuharibu Tanzania nzuri. Kwa Tanzania ya namna hii lazima matangazo ya jumuiya za kimataifa yawe ni kuitaja Tanzania katika uchumi wa juu juu juu zaidi.
Nawaona viongozi wa kesho wakiongoza Kwa raha. Uongozi jamii, polisi jamii, biashara jamii na Kila jambo linakuwa na muunganiko wakijamii.
Naamini ndoto yangu Kwa Tanzania ya namna hii inawezekana na itakuwa halisi katika macho yangu haya.
Ni ndoto Tamu ya Tanzania ya kesho.

Upvote
4