bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,679
Its wonder kila kitu kipo juu ukiuliza kwanini wanakwambia VITA sawa ni vita je serikali imekuja na mipango gani kwa hiyo mtaachia wafanyabiashara waendelee kupandisha bei za vitu kisa vita hakuna tamko la kukemea vitu kupanda bei bali kuna tamko la kubariki viendelee kupanda.
Kupanda bei kwa nishati ya mafuta ya mitambo sina shida sana na hapo hilo halikwepeki kwani mpaka sasa hatuna rasilimali hiyo nchini.
Twende kwenye mafuta ya kupikia.
Wengi wetu tunafahamu asilimia kubwa ya mafuta ya kupikia yanatokana na ufuta/alizeti kitu ambacho naamini serikali yetu ingeamua kutekeleza kwa vitendo SERA YA KILIMO KWANZA na hakika leo meli zingekua zinapishana bandari zetu kupakia mafuta ya kupikia na kupeleka makwao sijui ni wapi tunafeli.
Hatuna sababu za msingi mpaka sasa kama ni maeneo tunayo ya kutosha kinachokosekana ni userious, udhubutu, sera bora na Mipango mizuri, kweli tumeshindwa kuchagua mikoa miwili hata mitatu ya kimkakati na kujaza wataalamu wa kilimo huko na kuwezekeza kwenye kilimo cha ufuta tu.
Namkumbuka sana Rais Magufuli kipindi cha Korona alisema wakati wao wanapiga Lock down sisi tulime sana mwisho wa siku watakuja kununua kwetu.
Tunaona Serikali karibia kila siku inajitahidi kutoa magari kwenye idara zake ila sijawahi ona angalau inatoa mitambo ya kilimo kama vile Trekta kwenye mikoa inayozalisha kwa wingi, angalau kila mkoa ungepata hata matrekta matatu na mkulima kutozwa kiasi kidogo tu cha gharama.
My Government tujitaidi kuwekeza kwenye kilimo kama tunavyosema kilimo ni uti wa mgongo wataalamu wetu watafute mbegu za muda mfupi za alizeti baada ya vita kwisha sio mbaya wakaenda hata Ukraine Kujifunza mbinu bora za kilimo cha alizeti.