Nchi za magharibi zaendelea kuchochea msukosuko wa madeni, licha ya ushahidi wote kuonyesha wao ni chanzo kikuu cha msukosuko huo

Nchi za magharibi zaendelea kuchochea msukosuko wa madeni, licha ya ushahidi wote kuonyesha wao ni chanzo kikuu cha msukosuko huo

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1729215141442.png


Hivi karibuni kiongozi wa Kanisa la Katoliki Papa Francis alihutubia mkutano wa Vatican kuhusu Msukosuko wa Madeni katika eneo la Kusini mwa Dunia", kwenye hotuba yake Papa alikemea vikali changamoto zinazotokana na msukosuko huo, hasa kusababisha taabu na dhiki, na kuwanyima mamilioni ya watu uwezekano wa mustakabali wenye heshima. Papa alipendekeza kuwa nchi zenye mzigo wa madeni upunguzwe na kuweka mustakabali mzuri kwa nchi za Kusini.

Alichokisema Papa si jambo jipya, amerudi tu kinachosemwa na wataalamu wa mambo ya uchumi na fedha kuhusu changamoto nyingi zilizopo katika nchi za kusini, ambazo zinaweza kutatuliwa kama mzigo wa madeni utapunguzwa. Kwa maana nyingine ni kuwa Papa anasema kutatua msukosuko wa madeni, ni moja ya suluhu muhimu za changamoto zinazozikabili nchi za kusini.

Tunapozungumzia changamoto ya madeni, ni wazi kabisa kuwa tunazungumzia nchi nyingi za Afrika. Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na benki ya dunia zinaonesha kuwa jumla ya deni la nje la nchi za Afrika, limelofikia zaidi ya dola za kimarekani trilioni 1.152. Lakini nchi za magharibi zimekuwa zinaitupia lawama China kuwa ndio chanzo kikubwa cha deni hilo, na kwamba China ndio inasababisha changamoto hiyo.

Wataalamu pia wanasema kuwa namba hazidanganyi. Utafiti uliofanywa hivi karibuni ya taasisi inayoitwa Debt Justice, inaonesha kuwa nchi za Afrika zina deni mara tatu zaidi kwa nchi za magharibi, kuliko deni lao kwa China, lakini pia riba zinazotozwa na nchi za magharibi ni mara mbili kuliko riba inayotozwa na China. Benki ya dunia pia imetoa ripoti yake kuwa asilimia 12 tu ya deni la nje la serikali za Afrika linadaiwa na wakopeshaji wa China, na asilimia 35 ni deni la wakopeshaji wa binafsi wa nchi za Magharibi.

Soma Pia: Hoja ya “China inamwaga pesa kwa Afrika” yanaonesha wivu wa nchi za magharibi


Ukiangalia kwa undani lugha inayotumiwa na nchi za magharibi dhidi ya China, yaani “mtego wa madeni” kimsingi unaweza kuona kuwa wakopeshaji wa magharibi ndio wanaweka mtego wa madeni. Sababu ni kuwa mara nyingi mikopo inayotolewa na taasisi za magharibi zinalenga kila kinachoitwa kujenga uwezo, (capacity building) eneo ambalo mara nyingi tija yake ni ndogo au inachelewa sana kuwa na matokeo, na kufanya kusiwe na uwezo wa kulipa deni linalotolewa.

Mikopo inayotolewa na China mara nyingi ni inalenga kinachoitwa kuendeleza uwezo (capacity development). Kwa uchambuzi wa haraka haraka ni kuwa mikopo inayotolewa na China kwa nchi za Afrika na nchi nyingine za kusini, kimsingi inaelekea kwenye maeneo ya kiuchumi yanayoongeza uwezo wa nchi hizo kujiendeleza na kulipa madeni hayo, na ile inayotolewa na nchi za magharibi kimsingi inafanya wakopaji kuendelea kuhudumia madeni hayo milele bila kuwa na njia rahisi ya kulipa, na kujikita kwenye mzunguko wa kulipa deni, yaani mtego wa deni.

Mkuu wa Sera kwenye taasisi ya Debt Justice Bw. Tim Jones, amesema mara kwa mara kuwa wanasiasa wa nchi za magharibi wamekuwa wanailaumu China kwa msukosuko wa madeni barani Afrika, lakini ukweli ni kwamba taasisi zao za fedha, ndio wanawajibika zaidi. Na China ilipokuwa mstari wa mbele katika kuitikia mpango wa kusimamisha deni kwa nchi za Afrika wakati wa janga la COVID uliotolewa na kundi la G20, wakopeshaji binafsi wa magharibi waliukataa mpango huo, lakini China ilitekeleza mpango huo na kuleta ahueni kubwa

Alichokisema Papa Francis licha ya kuwa hakuitaja nchi yoyote, ni wazi kuwa kinaonesha kuchukizwa na mfumo wa kimagharibi wa ukopeshaji unaosababisha changamoto kwa nchi za kusini. Kama nchi hizo za magharibi na taasisi zake za ukopeshaji zikiendelea kuepusha lawama bila kuchukua hatua, hakutakuwa na mabadiliko ya maana.
 
Back
Top Bottom