Supermarket nyingi nchi za wenzetu hupunguza bei ya bia na bidhaa nyingine zikikaribia tarehe ya “best before” ili zisitupwe na kupunguza waste.
Mfano mimi nilienda supermarket nikakuta bia imewekewa sticker ya discount kubwa kabisa ili iuzwe haraka kabla muda haujaisha.imagine punguzo la 70% nilivyo mlaku wa bia nimezibeba bia karibia 20 zikae tu kwenye fridge
Lakini Tanzania sijawahi kuona mfumo huu ukiwa common sana kwenye supermarket nyingi. Mara nyingi bidhaa zinabaki bei ileile hadi mwisho.
Wabongo wengi hatuna utaratibu wa kusoma taarifa za kuisha matumizi ya bidhaa,
Kuna siku nilipewa sprite ime expire miezi mitatu nyuma,niliwaambia jamaa kama hawatatoa hizo bidhaa zilizoharibika ningewashtaki,sijui ata kama walifanya hivyo.
Hata huku ndio hivyohivyo..Zile biscut unazoziona feri na baadhi ha products mitaani Supermarkets huwa wanazitoa kwa promosheni zikikaribia kuexpaya.Sisi tulikuwa na supermarket na tulikuwa tunafanya hivyo bidhaa ikikaribia kuisha muda tunairudisha Godown kuna wadau wetu tynawapigia simu huwa wanakuja kuchukua