JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Ulaya imeeleza umuhimu wa demokrasia kazini, ukionesha faida kwa wafanyakazi, kampuni na jamii kwa ujumla.
Utafiti umeeleza kuwa Demokrasia katika sehemu ya kazi humfanya mfanyakazi awe na sauti ya kutoa maoni yake ambaye yanaweza kukuza zaidi ufanisi wake. Vilevile humfanya aweze kuipenda kazi yake zaidi.
Nchi zenye Demokrasia kwenye maeneo ya kazi zimeonekana kuwa na uchumi mkubwa zaidi kulinganisha na nchi zisizo na demokrasia.
Wafanyakazi wanaonekana kuwa na ubunifu zaidi wakiwa na Demokrasia. Wanakuwa na uwanja mpana zaidi wa kuboresha mawazo yao.
Muhimu zaidi, nchi zenye Demokrasia katika maeneo ya kazi vilevile zinakuwa na usawa. Usawa ambao ni nguzo kubwa ya kukuza maendeleo ya Demokrasia.
Nchi zinazoongoza kwa Demokrasia ni Norway, ikiufuatiwa na Iceland, Sweden, New Zealand na Canada.
Je, sehemu unayofanya kazi kuna demokrasia, na unazungumziaje kuhusu umuhimu wa demokrasia kazini?
Upvote
0