Nchi zenye wachezaji kama watanzania hazifai kusajili wachezaji wake

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Ukisikia timu inasajili mchezaji kutoka South Africa,Zimbabwe,au Uganda,utagundua kuwa ina watu wasio na uelewa wa kutosha kuhusu mpira na vipaji vya mpira.

Nasema hivi kwa nini?
Hapa Tanzania kuna wachezaji wana vipaji vikubwa sana kuliko wachezaji wengi wenye majina.Tofauti iliyopo ni kuwa hawa wetu wana vipaji ila hawajielewi.Ukichukua wachezaji kutoka nchi hizo hapo juu wana vipaji vya kawaida ila wanajielewa.

Hata hivyo bahati mbaya ni kwamba,suala si kipaji na kujielewa pekee.Bali lazima kuwe na tabia ya kutokubali kushindwa( Fighting sprit)Hiki ndicho kitu kikubwa kwenye mpira kuliko kupaji.Unaweza kuwashinda watu wenye vipaji kama tu una fighting spirit.
Wachezaji wa aina hii,wanapatikana nchi kama Congo.Kuna aina ya wachezaji wanaotakiwa kwenye soka la kisasa.Soka linalohitaji watu wanaojituma na kuweka energy zao zote hadi sekunde ya mwisho.
Si wa south ambao ni wavivu na wana mpira wa show off.

Sehemu bora ya kusajili wachezaji kama hao ni Congo na nchi za magharibi.Siyo huko Afrika kusini
 
Hata mifano ya hao wenye vipaji na hawajielewi hujaweka

Na hao wanaotoka nje ya Tanzania na hawana vipaji kama nani ?

Anyway mwenyekipaji hata kama hajielewi kitaonekana tu. Na kusajili kutoka nje hakuepukiki mzee khaa mtu kama waziri Jr anapewa nafasi ya kucheza lakini deliverance yake ni poor.
 
Sina tatizo na kusajili kutoka nje.Tatizo unasajili kutafuta nini?
Ninachoona kinakosekana hapa kwetu ni vitu viwili. Kujituma na kutojitambua.

Utagundua kuna wengi wana vipaji na wakijituma kuna kitu unakiona.Bahati mbaya utawaona wanajituma tu pale wanapocheza na timu kubwa kama Simba au Yanga na wanaweza kupata matokeo.Sasa suala la kutokujitambua linawafanya waone kazi yao kubwa inaishia kuonesha uwezo kwa timu kubwa tu.Lakini kama wangejua kuwa wanapaswa kuwa na consistency ili waonekane na timu kubwa,wasingejilegeza baadhi ya mechi
 
Mchezaji gani msauzi amewahi sajiliwa hapa bongo au umeamua kuongea tu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…