GE2025 Nchimbi: Mwambieni Mpina arudi CCM haraka. Akirudi nitampokea mwenyewe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa macho yangu ya rohoni, image ya Urais ilishaanza kumvaa Mpina, yaani alikuwa anaanza kufanania hivi. Na hii nadhani ndo imewashitua CCM.

Kwa usalama wake Mpina, ni bora asirudi CCM, maana tayari ameonekana ni mtu ana fit kupata madaraka makubwa na ameonesha kuwa ambitious, hiyo ni hatari sana
 
Same birds...
 
Ndugu zangu Watanzania,

Soma hapa👉Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi amemuomba Luhaga Mpina arudi haraka kwenye Chama chake cha awali CCM na ameahidi atampokea kwa mikono yote miwili.

Akiongea akiwa katika Jimbo la Kisesa Mkoani Simiyu leo September 02,2025, Nchimbi amesema “Atakayempigia simu Mpina amwambie Kaka yake mkubwa alipita hapa na mwambieni hasiponipigia kura atakuwa amekosa adabu ya kisukuma kabisa maana nilipopita si aliwaambia kwamba Mimi Kaka yake, mwambie Kaka yako alipita hapa na anasubiri akirudi tena anataka urudishe hiyo kadi ya Chama chako kipya urudi CCM na Mimi nitapokea kadi ya Mpina Mimi mwenyewe simtumi Mtu yoyote”

Mpina alikuwa Mbunge wa Kisesa kupitia CCM ambapo baadaye alishindwa kwenye mchakato wa kura za maoni na akahamia ACT Wazalendo ambako aliteuliwa na Chama hicho kugombea Urais lakini Msajili wa Vyama vya Siasa amemzuia kugombea baada ya Mwanachama wa ACT Monalisa Ndala kupeleka malalamiko akidai Mpina hajatimiza vigezo vya kugombea na sasa kesi ya suala hilo ipo Mahakamani.
#MillardAyoUPDATES

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Wewe maskini ya Mungu hakuna hata wa kukuita japo una kadi ya CCM. Baraka ya kutoa machozi ya furaha tu 😀 😀 😀
 
mpina ni poyoyo sana wa kisiasa
 
Kesho polepole ANAUNGURUMA mwambie nchimbi akae tayar
 
War Retreat......Mission Failed.

NRNE
 
Wamempiga mazonge ili haya maneno yaje kutimia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…